Na Abdi Moalim, Mogadishu
Baada ya mikutano mingi wiki hii katika mkutano wa London kuhusu
Somalia, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na mawaziri wake wamerudi
nyumbani wakiwa na ahadi kutoka jumuiya za kimataifa ya takribani dola
milioni 450 kusaidia miradi mingi.
Wakaazi wa Mogadishu waliandamana mitaa
Jumanne (tarehe 7 Mei) kuonyesha kuunga mkono mkutano wa London kuhusu
Somalia. [Abdi Said/Sabahi]
Katika hotuba yake ya ufunguzi kwenye mkutano huo, Mohamud alilinganisha
Somalia na mti mchanga uliooteshwa huko Villa Somalia ambao unahitaji
kumwagiliwa. kutunzwa na kulindwa dhidi ya wanyama.
"Kipindi cha kwanza cha ukuaji mara zote ni chenye hatari sana, ambapo msaada mkubwa na ulinzi unahitajika," alisema.
"Tunahitaji ulinzi dhidi ya wale wanaojaribu kutuangamiza kabisa,"
alisema. "Kwa pamoja, tunaweza kufanya Somalia kuwa imara tena -- mti
mrefu uliosimama katika msitu wa Afrika ukiwa na mizizi mirefu
uliokingwa kwa usalama katika kanda yake na kutoa kivuli kwa watu wake
wakati wakijenga tena maisha yao."
Waziri Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon
akipunga mkono kwa wakaazi wa Mogadishu waliojitokeza Jumanne (tarehe 7
Mei) kuonyesha kuunga kwao mkono mkutano wa kimataifa kuhusu Somalia
huko London. [Abdi Said/Sabahi]
Jumuiya za kimataifa zilijibu mwitikio wa Mohamud kwa kuahidi mamia ya
mamilioni ya dola. Pia ziliidhinisha mipango ya kina yaliyowasilishwa na
mawaziri wa Somalia, na kuahidi utaalamu na ufadhili wa fedha ili
kuzitekeleza.
Kwenye mkutano huo, serikali ya Uingereza iliahidi dola milioni 277,
ambapo dola milioni 54 zitaelekezwa kwenye miradi kushughulikia
changamoto ya usalama wa Somalia na serikali, na dola milioni 223
zitasaidia Somalia kukabiliana na njaa kwa siku zijazo.
Comments