Bendi
iliyokuja kwa kasi na inayoendelea kutamba hapa nchini kwa sasa Skylight Band
inatazamiwa kuwa kivutio kikubwa katika tamasha la filamu nchini
ZIFF.
Bendi
hiyo inayoongozwa na mwanadada Aneth Kushaba, AK 47 inajipanga kupiga shoo kali
ya karne katika Tamasha hilo la 16 la filamu za kimataifa litakalofanyika ndani
ya Ngome Kongwe mjini Zanzibar.
Akizungumzia
ushiriki wao Aneth Kushaba alisema “Zanzibar patakuwa hapatoshi, tumefurahi
kupata fursa ya kutumbuiza ZFF na tunasubiri kwa hamu kubwa kujitangaza
kimataifa”.
Skylight
inayoundwa na wanamuziki kama Sam Machozi, Jonicho Flower na wengine kibao pia
kwa sasa inatamba na vibao kama Karolina, Wivu, Nasaka Dough, na wimbo wao mpya
Mbeleko.
Comments