Nje ya mochwari ya Serikali Hillbrow
Johannesburg ulikohamishiwa mwili wa Ngwea.Picha za chini ni Watanzania wakiongozwa na
Kinje Ngomale Mwiru wakitazama sample ya majeneza mbalimbali ili wajue
la kununua, hapa walikua na mfanyabiashara wa kampuni ambayo pia huwa
inashughulika na kusafirisha miili ambapo gharama yake ni zaidi ya
milioni nne na nusu
Watanzania waishio Afrika ya Kusini walipokutana juu ya msiba wa Albert Mangwea.Kifo cha Ngwear kimetokea juzi nchini humo baada ya kukutwa chumbani kwake akiwa tayari amefariki na msanii mwenzaki M to the P akiwa hajitambui.
Millard Ayo akifanya interview na promota
Mtanzania ambae alikua tayari na kazi ya show tatu za ziada ya Ngwea
kabla hajafariki, zilipangwa kufanyika siku kadhaa zijazo.…
Mwili wa marehemu Ngwair bado upo mochwari ya Serikali Hillbrow
Johannesburg na leo ndio unafanyiwa uchunguzi ili kujua nini sababu za kifo chake.Pia taratibu za kuuleta mwili Tanzania ziweze kuendelea.
R.I.P Albert Mangwea
Habari na Millard Ayo akiwakilisha clouds fm Afrika ya Kusini ili kupata taarifa za kina juu ya msiba huu.Chanzo:Dina marios.com
Comments