Mkuu wa
Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja akikagua Guard ya
Heshima iliyoandaliwa kwa ajili yake kabla ya kuanza zoezi la Uvalisha
Nishani kwa Maafisa na Askari wa Magereza toka Mikoa ya Kanda ya
Kaskazini katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro
Mkuu wa
Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (kulia) akimvalisha
Nishani ya Utumishi Uliotukuka Kazini, Mkuu wa Magereza Mkoa wa
Kilimanjaro, ACP Hamis Nkubasi. Jumla ya Maafisa na Askari 30 kutoka
Mikoa ya Kanda ya Kaskazini wamevalishwa Nishani mbalimbali.
Mkuu wa
Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (katikati waliokaa)
akiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa Nishani mara baada ya zoezi
la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka
Mikoa ya Kanda ya Kaskazini l katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga,
Moshi, Kilimanjaro. Picha na Felix Mwagara.
Comments