Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema
kuwa, Marekani inafanya njama za kukwamisha maendeleo yaliyopatikana
katika mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa.
Fawzi Barhoum amesema kuwa, serikali ya Marekani inafanya njama za
kusambaratisha juhudi za Misri zenye lengo la kuhakikisha kunapatikana
maridhiano ya kitaifa baina ya makundi mbalimbali ya Palestina na
kuhitimishwa hitilafu zilizopo baina ya Hamas na Fat'h.
Fawzi Barhoum ameashiria safari ya John Kerry Waziri wa Mashauri ya
Kigeni wa Marekani katika Mashariki ya Kati na kusema kwamba, safari
hiyo haitakuwa na ujumbe mpya kwani lengo lake ni kuuokoa utawala wa
Kizayuni wa Israel na migogoro ya kisiasa na kuishinikiza serikali ya
Mamlaka ya Ndani ya Palestina.
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS
amesisitiza kuwa, serikali ya Marekani inafanya njama za kutaka
kulitokomeza faili la maridhiano ya kitaifa.
John Kerry Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, Alkhamisi ijayo
atafanya safari Mashariki ya Kati kwa shabaha ya kuendeleza mazungumzo
yake na viongozi wa Israel na Mamlaka ya Ndani ya Palestina ili kujaribu
kuzikinaisha pande mbili zirejee katika mazungumzo ya mapatano.
Chanzo: kiswahili.irib.ir
Chanzo: kiswahili.irib.ir
Comments