Na Adnan Hussein, Mogadishu
Serikali ya Somalia inapanga kupeleka kikosi imara cha askari polisi
1,300 mwishoni mwa mwezi wa Mei ili kusaka wanachama wa al-Shabaab
Mogadishu yote wakiwa na lengo la kuzuia mashambulizi na mauaji dhidi ya
wanaharakati wa amani, vikosi vya usalama na maafisa wa serikali.
Askari wa Kikosi cha Polisi cha Somalia
wakitoa saluti tarehe 18 Januari kabla ya kuingia ndani ya ndege
kuelekea Djibouti kushiriki katika kozi ya mafunzo ya miezi mitatu. [Na
Stuart Price/AU-UN IST/AFP]
"Miongoni ya kazi za kikosi chetu kipya ni kuweka sheria ya kutotoka
nje, kuendesha misako, kuzuia mashambulizi, kulinda viongozi wa umma na
kulinda [vituo vya polisi katika vitongoji]," Waziri wa Mambo ya Ndani
na Usalama wa Taifa wa Somalia Abdikarim Hussein Guled aliiambia Sabahi.
"Askari wake watakuwa tofauti na vikosi vyengine kwa sababu ya sare zao
za kipekee, vifaa na magari, pamoja na sababu ya kuwa wao watakuwa
wakipokea mafunzo yanayoenelea ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha
viwango vyao vya ukakamavu."
Kitengo cha polisi maalumu tayari kilishapatsa mafunzo nchini Somalia na
nje katika matayarisho ya kuaanza kazi kwao, Guled alisema. Watapelekwa
katika magari 120 yaliyopakwa rangi inayozitofautisha na wakiwa na zana
zenye redio za kisasa na zana za kutoa tahadhari.
Kitengo hiki ni sehemu ya kampeni ya serikali ya shirikisho ili
kuimarisha usalama na operesheni za kupambana na ugaidi mjini Mogadishu.
Comments