Ethiopian airlines yadhamini Tamasha la Filamu la Kimataifa - Zanzibar International Film Festival (ZIFF) ü Skylight Band Kuburudisha ZIFF
Kampuni ya usafiri wa anga..
Ethiopian airlines imejitokeza kudhamini Tamasha la 16 la filamu Tanzania, ZIFF
linalotazamiwa kufanyika Zanzibar, June 29 hadi July 7, 2013. Meneja na
Mkurugenzi msaidizi wa Tamasha hilo Daniel Nyalusi maarufu kwa kifupisho cha Dean
alisema wanajisikia furaha sana kushirikiana na Kampuni hiyo, na kwamba
anatarajia ushirikiano huo utafungua njia kwa makampuni mengine.
Aidha Dean alisema Ethiopian Airlines
ndio wamekuwa wadhamini rasmi wa usafirishaji wa watengenezaji
filamu na wageni wote wa ZIFF kimataifa na kuongeza kuwa Tamasha la ZIFF 2013
linatarajiwa kufana zaidi kutokana na maandalizi yake na udhamini huu mkubwa wa
Ethiopian Airline.
Pamoja na Ethiopian Airlines kampuni
nyingine iliyojitosa kwenye udhamini wa Tamasha hilo ni ZUKU TV, hii itakuwa
mara ya pili kampuni hii kushiriki katika kuunga mkono Tamasha hilo, ambalo
kwa miaka 16 iliyopita limesherehekea kazi za sanaa nchini na
kuwezesha uzalishaji wa filamu hapa Tanzania na duniani kote.
Akizungumziaa
ushirikiano huo, Meneja wa ZIFF, Daniel Nyalusi alisema “ ZUKU inadhamini dola laki
moja kila mwaka kwa miaka 10 kuanzia mwaka jana na itaangalia jinsi ya kupanua
udhamini wake kadri muda unavyoendela” Dean alisema “Tunakaribisha wadhamini
wengine kushirikiana na ZIFF na matumaini yetu ni kwamba wadhamini wataweza
kufaidika kutokana na ushirikiano huu kwani ni nguzo ya masoko ya ubunifu kwa
ajili ya wawekezaji na wafanyabiashara ambao wana maono kwa ajili ya ukuaji wa
uchumi na ajira katika sekta zote, hasa utalii na burudani. Kwa
kazi ya kukuza sekta ya burudani, ZIFF na Makampuni shiriki yatasaidia kujenga
ajira kwa watengenezaji wa filamu, wazalishaji na watendaji katika kanda nzima.”
Tamasha la ZIFF hupokea wageni zaidi ya 6000 toka nje kila mwaka na zaidi ya
watu 45,000 wakati likiendelea Zanzibar.
Comments