Na Rajab Ramah, Nairobi
Kushindwa kutekeleza mfumo wa elimu ya kawaida yenye sifa zilizowekwa
katika kiwango kilichokubalika ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC) kumezuia mtiririko wa fursa za rasilimali watu na biashara, wadau
wasema.
Mhandisi wa Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya
Kenya akisimamia mifumo katika chumba cha kudhibiti umeme unaozalishwa
kutokana na maji ya bwawa. Kwa kuwa na viwango vya elimu vyenye uwiano,
wahandisi wangeweza kufanya kazi katika nchi za Afrika Mashariki ambazo
zina uhitaji mkubwa. [Tony Karumba/AFP]
"Kila nchi ina viwango tofauti katika kuajiri wafanyakazi kwa sababu ya
kutofautiana kwa mfumo wa elimu," alisema Patrick Obath, mjumbe wa
Baraza la Biashara la Afrika Mashariki, asasi mama ambayo inawezesha
ushiriki wa sekta binafsi katika mchakato wa kujumuisha EAC.
"Jambo hili linazuia uwezo wa kuwepo, mfano, raia wa Uganda kufikiriwa
katika kazi nchini Kenya au Tanzania na kinyume chake," aliiambia
Sabahi. "Hili linazuia utekelezaji wa itifaki ya soko la pamoja."
EAC, makao makuu yako Arusha, Tanzania, ni asasi baina ya serikali
ambayo inadhamiria kupanua ujumuishaji wa kiuchumi, kisiasa na
kiutamaduni baina ya Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.
Obath alisema kushindwa kurahisisha fursa za ajira nje ya mipaka
kumefanya mchakato wa ujumuishaji wa EAC na ushindani wa kikanda kwa
ujumla kwenda taratibu.
Comments