LAGOS, Nigeria
Nyota wa filamu nchini Nigeria, Monalisa Chinda amesema moja ya mambo anayoyajutia katika maisha yake ni kuachika kwa mumewe.
Monalisa amesema yeye ni binti wa kwanza katika familia yao na anatoka kwenye familia ya kitajiri na haijawahi kutokea kwa mtoto wa kwanza kuachika.
"Lakini lilikuwa ni suala la maisha na kifo, vinginevyo, ningeweza kurejea kwa mume wangu na kuifanya ndoa yangu idumu. Nilijaribu kuifanya iwe hivyo, lakini haikuwezekana,"alisema.
Monalisa alisema hicho ndicho pekee anachokijutia katika maisha yake, kumtunza na kumkuza mwanaye bila kuwa na baba.
"Inauma sana. Lakini ninapaswa kuizoea hali hii,"alisema Monalisa.
Pamoja na kuachika, Monalisa alisema bado anaamini yapo mapenzi ya kweli na ndiyo yanayowafanya binadamu kuendelea kuwepo duniani.
Monalisa alisema angependa kuolewa kwa mara ya pili kwa vile hafurahii kuishi maisha ya upweke.
"Lakini kwa vile sina mtu kwa sasa, napaswa kuyazoea maisha haya,"alisema.
Monalisa alisema ni vigumu kwa sasa kusema ni lini anatarajia kufunga tena ndoa, lakini alisisitiza kuwa, anapendwa na anapenda kuwamo katika mapenzi.

Comments