Walimu waliojitolea kubeba mtoto katika
shule BRIARWOOD Elementary baada ya kuathirika vibaya kwa kimbunga
kilichoharibu shule ya kusini mwa Oklahoma City. (Photo.dailymail.co.uk)
Kimbunga kikubwa cha Tornado kimeukumba mji wa Oklahoma mapema leo
Jumatatu na kubomoa vitalu vya nyumba, shule mbili na kuua takribani
watu 91 ikiwa ni pamoja na watoto 20, viongozi wa mitaa wamearifu.
Rais Obama amesikitishwa na tukio hilo na kuliita janga kubwa ambapo
Kikosi cha uokozi kimeendelea na jitihada za kutafuta manusura katika
mabaki ya majengo.
Waokuaji wakiendelea kuogoa baadhi ya
watotho waliokumbwa vibaya kwa kimbunga katika Shule Plaza Towers
Elementary kufuatia kimbunga kilichoathiri vibaya huko Moore, Oklahoma.
(Photo.dailymail.co.uk)
Ofisi ya mtabibu wa serikali imetoa taarifa ya karibuni kuhusu idadi ya
waliopoteza maisha lakini idadi hiyo inaongezeka kwa kasi, wakati kikosi
cha huduma ya dharura wamesafisha mabaki yote ya nyumba zilizobomolewa
pamoja na shule katika kitongoji cha Moore mjini Oklahoma.
Watabiri wa hali ya hewa wamearifu kuhusu uwepo wa upepo mkali wa maili
mbili, na helikopta ya habari za televisheni imenasa faneli zito
likipita katika vitongoji kadhaa.
Gavana wa Oklahoma Mary Fallin ameviambia vyombo vya habari kuwa
kimbunga hicho ni kikubwa zaidi kuwahi kutokea katika eneo hilo
akiongeza kuwa majeruhi ni wengi na uharibifu mkubwa wa miundo mbinu
umefanyika.
Naye mkuu wa polisi katika kitongoji cha Moore Jerry Sillings amewataka
wakazi wa kuondoka katika eneo hilo wakati masuala kadhaa ya kiusalama
yakifanyika.
Waathirika: Uendelezaji uwokoaji wa watoto katika Shule ya Plaza Towers Elementary huko Oklahoma (Photo.dailymail.co.uk)
Comments