Na Bosire Boniface, Garissa
Serikali ya Kenya inapanga kufufua askari wa akiba wa Kenya (KPR),
programu ya kutoa mafunzo na kuwezesha vikosi vya raia, kusaidia
kupambana na wanamgambo wa al-Shabaab kutoka ndani ya jamii huko
Garissa.
Askari wa Kenya akiangalia mkutano wa
hadhara wa chama cha Harakati za Demokrasia ya Njano huko Garissa tarehe
22 Februari. Askari polisi wa akiba ambao ni raia wenye silaha hivi
karibuni watasaidia kulinda amani katika mji huo, wakilinda dhidi ya
vitisho kutoka kwa al-Shabaab. [Will Boase/AFP]
Garissa imekuwa mahali pa mashambulio makubwa ya al-Shabaab nchini Kenya
baada ya vikosi vya ulinzi vya Kenya kupeleka vikosi Somalia Oktoba
2011.
Iliongozwa na Inspekta Jenarali David Kimaiyo na Katibu Mkuu wa Usalama
wa Ndani Mutea Iringo, Kamati ya Ushauri ya Taifa imekuwa ikichunguza
mfululizo wa mashambulio kama hayo mwezi Aprili. Wakati wa mkutano wa
tarehe 20 Aprili, kamati ilipendekeza kushirikisha raia katika mji wa
Garissa kwa ajili ya operesheni za kigaidi.
KPR iliundwa mwaka 1948 kusaidia polisi kudumisha sheria na kanuni nchini Kenya kote.
Mwaka 2004, aliyekuwa kamishina wa polisi Meja Jenerali Mohammed Hussein
Ali alivunja na kunyang'anya silaha KPR katika maeneo ya miji ya Kenya
baada ya maofisa wake kuhusishwa na uhalifu wa kutumia nguvu na rushwa.
Hata hivyo, aliendeleza jeshi hilo katika maeneo ya vijijini, kupambana
na wizi wa ng'ombe na ujambazi.
Comments