Katibu Mtendaji wa Necta Joyce Ndalichako
WAKATI Serikali ikitangaza kufuta
matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani
la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam,Prof.Rwekaza Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya
Kidato cha Nne.Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara
baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo
hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi
tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.Iweje leo Baraza
libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa
elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala. Habari za kuaminika
zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce
Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi
wake huo.Naye Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Philipo Mulugo alipotafutwa kwenye simu yake ya mkononi kuzungumzia suala hilo iliita bila ya kupokelewa na baadaye akatuma ujumbe mfupi akisema, "Sorry I'm busy call back later", alisema Mulugo kupitia simu yake ya mkononi.Inatoka http://mjengwablog.com
Comments