Mwenyekiti wa CCM kijiji cha Minyinga kata ya Mungaa jimbo la Singida mashariki, John Theodore Ghumpi (wa kwaza kushoto) akimhoji mbunge Tundu Lissu, ni kwa nini anatetea wahalifu ambao amedai wamejichukulia sheria mkononi kwa kukata kata ng’ombe zake sita.Ghumpi ni mume wa Mary John.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Mbunge wa jimbo la Singida mashariki kupitia CHADEMA, Tundu Lissu, amepata wakati mgumu baada mmoja wa wapiga kura wake kumtaka amweleze ni kwa nini amekuwa akijikita kutetea wahalifu wa wazi wazi.
Diwani wa CHADEMA kata ya Mungaa jimbo la
Singida Mashariki, Matheo Alex (wa pili kushoto aliyenyanyua mkono juu)
akiwa katika chumba cha mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida akisubiri
kusomewa shitaka lake la kukata kata ng’ombe sita mali ya Mary John
mkazi wa kijiji cha Minyinga kata ya Mungaa.Wa pili kulia ni mtoto wa
diwani Alex, Faraja na wa pili kushoto Bahati Sumbe (mwenye jacketi la
njano) wameunganishwa kwenye kesi moja na diwani Alex.
Mkazi wa jimbo la Singida mashariki, John Theodore Ghumpi alimbana
vilivyo Tundu ambaye ni mwanasheria maarufu, muda mfupi baada ya
kusimamia kesi ya diwani wa CHADEMA kata ya Mungaa Matheo Alex na
wenzake wawili wanaotuhumiwa kukata kata ng’ombe sita kwa shoka mali ya
Ghumpi.
“Kwa kifupi mimi sina ugomvi wo wote na CHADEMA wala na wewe Tundu, wewe
licha ya kuwa ni ndugu wa ukoo, wewe ni mbunge wangu pia. Sasa
unapojikita kubariki uhalifu kama huu wa kukata kata ng’ombe
wangu,kwangu mimi unanipa wakati mgumu mno kukuelewa”,amesema Ghumpi.
Hata hivyo,Tundu alisema kuwa washitakiwa na walalamikaji katika kesi ya
kukata kata ng’ombe sita,wote ni wapiga kuwara wake na wananchi wake wa
jimbo la Singida mashariki,na hivyo ana wajibu wa kuwatumikia kwa
usawa.
Kutokana na kibano hicho,wakili anayewatetea washitakiwa hao watatu,
Tundu Lissu,alilazimika kufuatana na Ghumpi kwenda kijiji cha Minyinga
kuangalia ng’ombe wanaodaiwa kukatwa katwa na wateja wake akina Matheo.
Comments