SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua mwamuzi kutoka Afrika Kusini kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na wenyeji Morocco (Lions of the Atlas).
Mechi hiyo ya kundi C itachezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco kwenye Uwanja wa Grand kuanzia saa 3 kamili usiku kwa saa za Morocco. Mwamuzi atakayechezesha mechi hiyo ni Fraser Daniel Bennett.
Bennett atasaidiwa na Thusi Zakhele Siwela pia wa Afrika Kusini, wakati mwamuzi msaidizi namba mbili atakuwa ni Marwa Range kutoka Kenya. Mwamuzi wa akiba (fourth official) ni Lwandile Mfiki wa Afrika Kusini.
Comments