Na Abdi Said, Mogadishu
Kampeni ya Kitaifa ya Saudia kwa Kuwasaidia Watu wa Somalia imeahidi
kutoa mfuko wa msaada wa kina wenye thamani ya dola milioni 24 kwa
miradi ya ujenzi mpya nchini Somalia, kwa mujibu wa Jumuiya ya
Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), ambao unasaidia kuratibu fedha hizo.
Mwanamke wa Somalia akitembea karibu na
kambi ya watu wa ndani waliokimbia makazi yao mjini Mogadishu tarehe 3
Mei. Sehemu ya msaada wa Saudia ulioahidiwa Somalia utatumiwa kuwapa
makazi watu waliokimbia makazi yao. [Na Tobin Jones/AU-UN IST/AFP]
Msaada huo utakwenda kwa mikoa yote ya Somalia na utaelekezwa katika
sekta za elimu, afya, kilimo pamoja na kuwarekebisha watu waliokimbia
makazi yao na katika hali zote za ustawi wa jamii, OIC ilisema katika
taarifa hapo tarehe 12 Mei.
Wigo wa mfuko wa misaada na ushirikishwaji wa asasi zisizokuwa za
kiserikali, wazee wa kikabila, tawala za mikoa na serikali ya shirikisho
katika kuamua miradi gani ya kutekeleza inaashiria mtindo mpya wa
utoaji misaada nchini Somalia.
Lengo la msaada huu ni kukuza ujenzi mpya wa Somalia kupitia miradi
kadhaa inayoungwa mkono na Saudia, ambayo itaanza katikati ya mwezi wa
Juni, alisema Mohamed Idle Sabrie, naibu msimamizi wa ofisi ya OIC mjini
Mogadishu.
Kiasi cha watu 500,000 watafaidika na msaada wa fedha, ambao utakamilika
ndani ya miezi 18. Awamu ya kwanza itazingatia miradi ya mjini
Mogadishu, Sabrie alisema.
Comments