Mh Tundulisu akitoa Vyeti kwa wana chaso katika Haflahio,
WAANDISHI wa habari wapo katika hatari kubwa ya kutoweka nchini kutokana na kuandika maovu yanayofanywa na viongozi wa serikali.
Haya yamezungumzwa na Mbunge wa Singida
Mashariki na mnadhimu Mkuu wa kambi ya upinzani Tundu Lissu katika
mahafali ya shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu Mkoa wa Iringa (CHASO)
katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria kilichopo katika Manispaa ya Iringa.
Lissu alisema waandishi wa habari wapo
katika hatari ya kutoweka hasa kwa kuuawa kutokana na ukweli wao
wanaouandika hasa kuyaweka madudu ya baadhi ya viongozi wa serikali.
Alisema hasa katika ripoti ya uchunguzi
ya mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi ya tume iliyoundwa na
vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) inaonesha wazi juu ya
hatari walionayo waandishi wa habari.
Comments