Spika wa bunge Mh. Anne Makinda ameliahirisha bunge kwa dharura kupisha
kamati ya kudumu ya kanuni za bunge kukutana kwa ajili ya kuijadili
hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliyokuwa ikisomwa bungeni kwa madai
ya kuwa na baadhi ya maneno ya uchochezi na baadae kutoa maamuzi ya
kuondolewa kwa maneno yote yaliyoko katika ukurasa wa kwanza hadi 14 wa
hotuba hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu
Comments