RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE
KUZINDUA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA YA DODOMA – IRINGA YENYE UREFU WA
KM 260 (SEHEMU ZA DODOMA – FUFU ESCARPMENT, FUFU ESCARPMENT – MIGORI NA
MIGORI – IRINGA) KWA KIWANGO CHA LAMI TAREHE 22 MEI, 2013
Wizara ya Ujenzi inapenda kutoa taarifa kwa Umma kwamba, tarehe 22 Mei,
2013 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete atakuwa mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa miradi
ya ujenzi wa barabara kama ifuatavyo:-
1) Tarehe 22 Mei, 2013 Asubuhi kuweka jiwe la msingi sehemu ya Dodoma – Fufu Escarpment (km 93.8) katika eneo la Dodoma Mjini.
2) Tarehe 22 Mei, 2013 Mchana kuweka jiwe la msingi sehemu ya Fufu
Escarpment – Migori (km 70.9) na Migori – Iringa (km 95.3) katika Kijiji
cha Migori Wilayani Iringa Vijijini.
Barabara ya Iringa – Dodoma ni sehemu ya barabara muhimu ijulikanayo
kama “Great North Road” inayoanzia Capetown Afrika ya Kusini hadi Cairo,
Misri kupitia Tanzania. Nchini Tanzania inaunganisha Miji ya Tunduma
(mpakani na Zambia), Mbeya, Iringa, Dodoma, Arusha na Namanga (mpakani
na Kenya).
Comments