Dodoma. Rais Jakaya Kikwete
amebainisha kuwa vurugu za kidini na kisiasa zinazotokea nchini, zina
uhusiano na watu wa nchi za nje.
Alitoa kauli hiyo jana kwenye ibada
maalumu ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Mkuu wa Sitta wa Kanisa Anglikana
Tanzania, Dk Jacob Chimeledya.
Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi kwenye ibada hiyo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu.
“Wanaohamasisha vurugu hizo ni watu
wenye uhusiano ya karibu na watu wa nje ambao mambo yakiharibika nchini
watakuwa wa kwanza kupanda ndege, ilhali wakiendelea kutoa matamko ya
uchochezi wakiwa nje ya nchi wakati wengine wakiendelea kuumia,” alisema
Kikwete.
Ibada hiyo ilifanyika chini ya ulinzi
wa polisi na askari wa usalama, na ilihudhuriwa na Askofu Mkuu wa
Anglikana duniani, Justin Welby.
Rais Kikwete alisema... Soma zaidi.. http://www.mwananchi.co.tz
Comments