Na Julius Kithuure, Nairobi
Tangu mahakama ya Kenya ilipotoa hukumu kwa raia wawili wa Iran kwenda
jela kifungo cha maisha kutokana na mashtaka yanayohusiana na ugaidi
mapema mwezi huu, hali ya baadaye ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya
Nairobi na Tehran imekuwa wa mashaka, kukiwa na uwezekano wa kurudisha
nyuma matumaini ya Iran ya kupanua shughuli na uwepo wake kisiasa nchini
Kenya kwa miaka ijayo.
Sayed Mansour (katikati) na Ahmad Mohammed
(kulia), wote wawili ambao ni raia wa Iran, wanafungwa pingu mara tu
baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha jela hapo tarehe 6 Mei kutokana
na mashtaka yanayohusiana na ugaidi, ikiwa ni pamoja na kumiliki
iliyodaiwa kuwa milipuko kwa ajili ya kutumia katika mashambulio ya
bomu. [Simon Maina/AFP]
Mgogoro huo wa kidiplomaisa ulitokana na shambulio la ugaidi
lililoteguliwa nchini Kenya ambalo lililotolewa hukumu na mahakama
ambalo lilikuwa limepangwa na Ahmed Mohammed, mwenye umri wa miaka 50,
na Sayed Mansour, mwenye umri wa miaka 51, wote wawili raia wa Iran.
Wanaume hao wawili walikamatwa mwezi Juni mwaka uliopita nje ya Laico
Regency, hoteli yenye nyota tano inayomilikiwa na Mlibiya katikati ya
Nairobi, siku nane baada uchunguzi mkubwa uliofanywa na Kitengo cha
Polisi Kinachopambana na Ugaidi.
Tarehe 2 Mei, walitiwa hatiani kwa kumiliki kilogramu 15 za milipuko
yenye nguvu ya RDX, ambayo polisi waligundua kufukiwa kwenye uwanja wa
gofu. Mahakama ya Nairobi ilisema Mohammed na Mansour walishukiwa
kuhusika na ulipuaji bomu uliopangwa na mtandao wa kigaidi huko Mombasa
na Nairobi. Wanaume wote hao wawili walikana mashtaka hayo.
Lakini polisi wa Kenya walitetea uamuzi wao wa kuwakamata na kuwafungulia mashtaka Wairani hao wawili.
Comments