TAARIFA KWA UMMA
Kurugenzi
ya Habari na Uenezi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
inapenda kuutarifu umma kuwa viongozi kadhaa wa kitaifa, wakiongozwa na
Naibu Katibu Mkuu Bara, Mheshimiwa Kabwe Zitto watafanya ziara ya
kichama mkoani Tanga.
Ziara
hiyo itakayoanza Jumamosi, Februari 18, 2012, itaanzia Wilaya ya
Handeni, Korogwe, Mheza, Pangani, kisha Tanga Mjini. Katika maeneo yote
hayo Naibu Katibu Mkuu, Mheshimiwa Zitto atakagua uhai wa chama mkoani
humo, ambapo atafanya mikutano na wanachama wa CHADEMA.
Viongozi
hao wa CHADEMA pia watazungumza na wananchi mkoani Tanga katika
mikutano ya hadhara, kwenye maeneo yote hayo. Watatumia fursa hiyo
kuzungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa na yale ya maeneo husika.
MBali
ya kukagua uhai wa chama mkoani Tanga, katika ziara hiyo, Mheshimiwa
Zitto , pia atatumia fursa hiyo kuipeleka kwa wananchi na kuifafanua
hoja yake aliyoiwasilisha bungeni katika mkutano ulioisha hivi karibuni
juu ya zao za mkonge, ambapo baadhi ya wabunge wa Tanga, walisimama
kuipinga hoja hiyo.
Kurugenzi
ya Habari na Uenezi, inatoa wito katika maeneo yote ambayo msafara huo
wa CHADEMA utafanya mikutano, wananchi wahudhurie kwa wingi ili
wanufaike na ziara hiyo.
Imetolewa leo *jana* Februari 16, 2012, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Afisa Habari wa CHADEMA
Comments