Hafidh
Ameir mratibu wa TACAIDS mkoa wa Pwani akitoa mada katika semina ya
kuwajengea uwezo waandaji wa vipindi vya Redio na Watangazaji kwa Kanda
ya Mashariki inayofanyikwa kwa siku mbili kwenye hoteli ya Kibaha
Confernce Center Maili moja Mjini Kibaha. Waratibu
wa Ukimwi katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Lindi na Mtwara wapo
kwa ajili ya kuwaelezea masuala mbalimbali washiriki wa semina hiyo,
kuhusu maambukizi ya ukimwi na kupambana na janga zima la Ukimwi
linalotishia jamii na nyanja mbalimbali za kiuchumi nchini Tanzania
kutokana na kudhoofisha nguvu kazi ya Rasirilimali watu. Semina
hiyo imeandaliwa na Taasisi ya kuzuia ukimwi TACAIDS ikishirikiana na
kampuni ya Masoko Agencies (T) Limited ya jijini Dar es salaam na
tayari imeshafanyika katika kanda Kaskazini Arusha, Kanda ya Ziwa
Mwanza, Kanda ya Kati Dodoma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya na
sasa ni Kanda ya Mashariki Mjini Kibaha
Afisa
Uhusiano wa TACAIDS Grory Mzirai akitoa mada katika semina ya
kuwajengea uwezo waandaji wa vipindi vya Redio na Watangazaji kwa Kanda
ya Mashariki inayofanyikwa kwa siku mbili kwenye hoteli ya Kibaha
Confernce Center Maili moja Mjini Kibaha.
Lugano
Henry Meneja Mawasiliano na Mafunzo wa kampuni ya Masoko Agency
akizungumza katika semina hiyo inayofanyika kwa siku mbili katika
hoteli ya Kibaha Conference Center mjini Kibaha.
Bw.
Simon Keraryo Afisa Uhamasishaji (TACAIDS) naye alizungumzi mambo
kadhaa katika semina hiyo kama anavyoonekana katika picha.
Mmoja
wa watoa Mada ambaye pia ni mtangazaji wa ITV Bw. Godwin Gondwe
(kushoto) akiteta jambo na Meneja Mawasiliano na Mafunzo wa Kampuni ya
Masoko Agencies (T) Limited Lugano Henry.
Regina
Mwalekwa Mtangazaji kutoka Redio Clouds kulia kulia akiwa pamoja na
Jacqueline Chengula mtangazaji mwenzake kutoka Clouds wakiandika mambo
muhimu yaliyokuwa yakijitokeza wakati watoa mada wakiendelea na mada
hizo katika semina ya waandaaji wa vipindi vya redio na watangazaji
mjini Kibaha.
Comments