Mhe.
Ombeni Sefue Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza na
watanzania hawapo pichani wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa
na Jumuiya ya Watanzania waishiio Jijini NewYork na Vitongoji vyake,
kushoto kwake ni Mwenyekti wa Jumuia Bw. Hajji na kulia na Katibu, Bw.
Shaban
Mhe.
Balozi akiwa na Mke wake Bibi Anita Sefue( aliyeshika zawadi) ambayo
Jumuiya ya Watanzania walimkabidhi Balozi kama kumbukumbu ya kuwa
Mlezi wa Jumuiya yao, wengine katika picha ni viongozi wa jumuiya hiyo.
Mhe.
Balozi Ombeni Sefue, akiwa na Mke wake Bibi Anita Sefue katika picha ya
pamoja na sehemu ya watanzania waliohudhuria hafla hiyo
Na Mwandishi Maalum
New York
Balozi
wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ombeni Sefue
amesema,amejipanga vema kumsaidia Rais Jakaya Mrisho Kikwete na
Serikali kwa ujumla kupitia wadhifa wake mpya wa Ukatibu Mkuu Kiongozi
“Ninatambua dhamana hii ni kubwa, nzito na yenye changamoto
nyingi,lakini nimejipanga kutumia uwezo wangu , maarifa yangu na ujuzi
wangu wote kumsaidia Mhe, Rais na zinazoambatana na dhamana hiyo”.
Balozi
Ombeni Sefue, ameyasema hayo kumpongeza kwa wadhifa wake huo mpya,
hafla Watanzania waishio jijini New York na vitongoji vyake. Katika
hafla hiyo iliyofanyika siku ya alhamisi na kuhudhuriwa pia na Mke wa
Balozi,Bibi. Anita Sefue, amejipanga vema katika jukumu lake hilo
jipya. Amewashukuru kwa kutenga muda wao kuagana naye na vilevile
kumpongeza na kwamba ameguswa sana na tukio hilo. Katika mazungumzo
yake na watanzania hao, Balozi Sefue, amesisitiza umuhimu kwa wao,
kuzidumisha na kuziendeleza sifa ambazo zimeifanya Tanzania kuwa moja
ya kati nchi zinazoheshimika Barani Afrika.Akazitaja misingi ya dini,
rangi, kabila au jinsia “Watanzania tunaheshimika sana, tunaheshimika
kwa sababu tumeweza kuendeleza na kudumisha mambo makuu muhimu ambayo
ni utamaduni wetu wa kupendana,kuheshimiana, kutobaguana kwa misingi ya
dini, kabila, rangi au jinsia, wito wangu ninapoagana nanyi ni kwamba
muyaendeleze haya hasa nyie akasema Balozi Sefue.
Balozi
Sefue licha ya kuwahakikishia watanzania hao kwamba sifa hizo kuwa ni
umoja, mshikamano, upendo na kutobaguana kwa Na kusisitiza kwamba,
licha ya kuwa wao sasa wanaishi na kuendesha shughuli
zao
nchini Marekani. Lakini nyumbani kwao kwa asili ni Tanzania, na kwa
sababu hiyo wanaowajibu pia kuwafundisha mambo hayo watoto wao, ikiwa
ni pamoja na kuwarithisha mila na tamaduni za mtanzania na historia
nzuri wanakotoka.Akisisitiza umuhimu wa kusaidiana, Balozi Sefue
amesema watanzania wataweza
kusaidiana
pale tu watakapokuwa na Jumuiya inayowaunganisha.Na kwa sababu hiyo
akawataka kuienzi na kuendelea kuiimarisha Jumuiya yao ambayo yeyé,
licha ya kuwa mlezi wao lakini aliwasaidia sana yaliyopelekea
kuanzishwa kwa Jumuiya ya Watanzania New York na vitongoji yake.
Akasema ni kwa kupitia Jumuiya yao ambayo viongozi wake wamepatikana
kwa uchaguzi wakidemokrasia. kwamba ndipo mahali ambapo wanaweza
kubadilishana mawazo ya namna gani ya kusaidiana wao kwa wao lakini pia
kuwasaidia ndugu na jamaa zao waliowaacha nyumbani (Tanzania) na Taifa
kwa ujumla. “ Niwapongenze na kuwashukuru kwa kukubaliana nami pale
nilipowapatia ushauri wa kuunda Jumuiya yenu, ninashukuru kwamba tangu
kuasisiwa kwake mmekuwa mkiendelea vizuri.
Kwa
upande wao na wakizungumza kwa niaba ya watanzania wenzao, Mwenyekiti
wa Jumiya hiyo Bw. Hajji na Katibu wake Bw. Shaban Musemba,
wamemhakikisha Balozi Sefue kwamba kama sehemu ya kuenzi mchango wake
uliotukuka, watahakikisha Jumuiya yao haifi.Wakasema katika kipindi
kifupi ambacho Balozi amekuwa Mlezi wa Jumuia hiyo, wamejifunza mengi
kutoka kwake, na kwamba wanasikitika watakosa mchango wake wa mawazo,
ushauri na mwongozo. Lakini wanamtakia kila la kheri katika nafasi yake
hiyo mpya ya kumsaidia Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.Inatoka kwa mdau Mjengwa.
Comments