Frederick Katulanda, Mwanza
TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Mkoa wa Mwanza, leo
inatarajia kumpandisha kizimbani kigogo wa Baraza la Waislamu Tanzania
(Bakwata) mkoani Mwanza, kwa kosa la kuhujumu uchumi.
Habari
zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mwanza,
Christopher Mariba, zimedai kuwa kufikishwa mahakamani kwa Kigogo huyo,
kunatokana kutumia msamaha wa kodi wa Serikali kununua saruji kwa niaba
ya wafanyabiashara kwa jina la Bakwata, hivyo kukwepa kodi zaidi ya
Sh15 milioni kila mwezi mmoja.
Imeelezwa
kufikishwa mahakamani kwa kigogo huyo kunatokana na hujuma hizo kuanza
kufichuliwa na Gazeti la Mwananchi Jumapili, baada ya kutolewa mara ya
kwanza Januari 25, 2009 Takukuru walifanya uchunguzi wao na kubaini
kuwa kulikuwa na ukweli.
“Uchunguzi
wetu umekamilika, kama Mungu akijalia kesho (leo) tutamfikisha
mahakamani, sasa naomba mfike wenyewe mahakamani maana siwezi kuongea
sana juu ya masuala haya,” alisema Mariba.
Pia,
katika habari iliyoandikwa na Mwananchi Jumapili zilieleza katibu huyo
akiwa na dhamana ya kuongoza Bakwata, alishirikiana na wafanyabiashara
wa Mwanza kutumia jina la Bakwata kununua tani za saruji 2,298 kwa
Sh31,589,34.
Kipindi
cha wiki mbili wanadaiwa walinunua saruji kwa bei ya Sh16,500 kila
mfuko, kisha kuiuza kwa bei ya Sh19,000 yenye kodi sawa na
Sh43,651,913, hivyo kujinufaisha binafsi na kuikosesha Serikali mapato.
Ilielezwa
kuwa kiasi hicho cha fedha kiliwekwa katika akaunti namba 015101004917
iliyopo tawi la NBC Mwanza kabla ya kuingizwa kwenye akaunti hiyo
ilikuwa na salio la Sh474,045.45, lakini baada ya kuingia fedha hizo
zilitolewa kwa vipindi tofauti zikionyesha kwenda kwa Cement
Distributor kulipia ununuzi wa saruji.
Kulingana
na kumbukumbu ya nyaraka mbalimbali kutoka ofisi ya Bakwata mkoani
Mwanza ambazo gazeti hili imebahatika kuziona, Januari 3, mwaka huu
akaunti hiyo ikiwa salio la Sh474,045.45, ilionyesha kupokea
Sh8,680,000 na kiasi hicho kutolewa siku hiyo kwenda kwa Cement
Distributor.
Kiasi
kingine cha Sh11,085,163,00 kiliingia katika akaunti hiyo Januari 9,
mwaka huu lakini pia kilitolewa siku hiyo pia kikielekea kununua saruji.
Fedha
nyingine Sh11,824,176 ilingia katika akaunti hiyo na kutolewa siku
hiyo, hivyo kuifanya akaunti hiyo katika wiki mbili kupokea
Sh31,590,200 na kiasi hicho kutolewa na kuifanya akaunti hiyo kubakiwa
na salio la Sh474,045.45.
Kesi
hii itakuwa ya kwanza ya aina yake kwa viongozi wa dini kufikishwa
mahakamani wakikabiliwa na tuhuma za kusababisha Serikali kukosa mapato
www.mwananchi.co.tz.
Comments