Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanueli Nchimbi (kulia)
akizungumza na Rais wa Kituo cha Utamaduni na Uhusiano wa Kiislam
kutoka nchini Iran Dkt. Mohammed Basheir Khurrqmshad (kushoto) mara
baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam.
Pamoja na mambo mengine Rais huyo ameahidi kuendeleza ushirikiano kati
ya Tanzania na Iran katika sekta ya utamaduni na michezo ikiwemo
kusaidia kuleta makocha wa mchezo wa riadha.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Emmanueli Nchimbi
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali ya Iran
waliomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
Balozi
wa Irani nchini Tanzania (katikati) Movahhedi Ghomi akimweleza jambo
waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanueli Nchimbi
(kushoto) mara baada ya kumtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es
salaam. Kulia ni Rais wa Kituo cha Utamaduni na Uhusiano wa Kiislam
cha Iran Dkt. Mohammed Basheir Khurrqmshad.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZ
Comments