JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
TANZANIA KUWA MWENYEJI WA KONGAMANO LA KIMATAIFA KUHUSU UHIFADHI WA MBUGA ZA WANYAMAPORI
Wizara
ya Maliasili na Utalii inatoa taarifa kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa
Kongamano la Kwanza la Africa kuhusu Uendeshaji, Changamoto na Fursa
katika Uhifadhi wa Mbuga za Wanyamapori na Maeneo yaliyohifadhiwa (The
1st Pan-African Conference on Sustainable Tourism Management In
National Parks and Protected Areas: Challenges and Opportunities).
Kongamano
hilo la siku Tano limepangwa kufanyika katika Kituo ya cha Kimataifa
cha Mikutano cha Arusha (AICC) tarehe 15 hadi 19 Oktoba 2012. Washiriki
wapatao 300 kutoka nchi mbalimbali wanatarajia kuhudhuria.
Tanzania
imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO) kufuatia mkutano wake (UNWTO General
Assembly) ambao ulifanyika nchini Korea 2011. Katika Mkutano huo
Tanzania pia ilichaguliwa kuwa mjumbe katika Baraza la Utendaji
(Executive Council) la Shirika hilo, nafasi ambayo itakuwa nayo hadi
mwaka 2015.
Kongamano
hilo la Oktoba 2012 ni la kwanza na la aina yake litawakuwakutanisha
wahifadhi na wadau wa sekta ya Utalii ili wajadili namna ya kufanikisha
uhifadhi na utalii duniani. Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa
Kongamano hilo kutokanana na sifa nzuri na uzoefu ilio nao katika
kuanzisha na kuendeleza hifadhi za Taifa.
Tanzania
inategemea kupata manufaa kutokana na Kongamano hilo kwani washiriki
watapata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini na
hivyo kuvitangaza warudipo makwao. Pia watanzania watapata fursa ya
kuuza huduma mbalimbali kwa wageni watakaohudhuria Kongamano hilo, kama
vile malazi, chakula, burudani na usafiri.
Faida
nyingine ni kuwa, washiriki kutoka Tanzania watapata fursa ya
kubadilishana ujuzi na ueledi na wenzao watakaotoka nchi mbalimbali
duniani.
Wizara
inatoa wito kwa wanachi, wafanyabiashara na wadau wote kujiandaa
ipasavyo ili kunufaika na ujio huo wa Kongamano hilo la kimataifa
nchini.
Taarifa mbalimbali zitaendelea kutolewa kuhusu maendeleo ya maandalizi ya Kongamano hilo.
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
23 Februari 2012
Comments