Inasikitisha kwamba Bunge laweza kukaa wiki nzima na kujadili masuala
mbalimbali bila kutoa muda kujadili suala la mtikisiko katika sekta
Afya.
Siku ya kwanza ya Bunge nilisimama kutaka taarifa ya serikali kuhusu
mgomo wa madaktari na taarifa hiyo ijadiliwe na Bunge. Spika
akalojulisha Bunge kwamba Serikali imempa taarifa na itawasilishwa.
Bunge lika...ahirishwa siku bila kurejea. Kamati ya Uongozi ya Bunge
ilipohitaji taarifa ya Serikali, Serikali haikuwa na taarifa. Kwa hiyo
walifanya ujanja ujanja kuzuia mjadala wa mgomo wa madaktari.
Leo wabunge kwa mara nyingine wamesimama kutaka mjadala huu wa
dharura. Naibu Spika wa Bunge akatumia sababu za kiufundi kuzuia
mjadala. Inawezekana wabunge hawakuwaandaa wabunge kusimama kuunga
mkono hoja, lakini ni jukumu la Kiti kuona umuhimu na udharura wa
mijadala.
Hii inadhihirisha kwamba sasa Bunge kama Mbunge mmoja mmoja au kwa
ujumla wake na Taasisi ya Bunge imekosa mguso na Hali ya wananchi (out
of touch). Hali hii ni hatari sana. Wananchi wanapoona chombo
kinachowawakilisha hakitoi nafasi kwa masuala yanayowagusa, watachukua
hatua zao wao wenyewe na hivyo kuhatarisha utulivu wa nchi. Bunge
liache shughuli nyingine zote na kutoa fursa ya kupokea taarifa ya
serikali kuhusu madai ya Madaktari, kuijadili na kuazimia kwa
kuelekeza hatua za kutekelezwa na serikali.
Na Zitto Kabwe
Comments