RAIS JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI MATEMBEZI YA KUCHANGIA AKINA MAMA WENYE MATATIZO YA UGONJWA WA FISTULA CCBRT
Rais
Jakaya Kikwete wa nne kutoka kulia akishiriki katika matembezi ya
kuchangia shilingi Bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa jengo la akina
mama wenye matatizo ya ugonjwa wa Fistula katika hospitali ya CCBRT leo
asubuhi jijini Dar es salaam, matembezi hayo yameanzia katika hoteli ya
Golden Tulip na kumalizika katika Hospitali ya CCBRT Mikocheni,
matembezi hayo yameandaliwa kwa pamoja na kampuni ya Vodacom Tanzania,
Vodafone pamoja na hospitali ya CCBRT Kampeni hiyo inaitwa (Finde your Moyo).
Katika picha kutoka kulia ni Erwin Telemans Mkurugenzi mtendaji wa
CCBRT, Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Mwenyekiti wa
Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw. Wilbroad Slaa na kushoto kwa Rais ni
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hadji Mponda wakishiriki katika
matembezi hayo leo asubuhi.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa CCBRT, Brenda Msangi
katikati alipokuwa akipata maelezo mbalimbali wakati alipowasili katika
hospitali hiyo baada ya matembezi hayo, kushoto ni Dk. Brenda kutoka
hospitali ya CCBRT.
Bendi ya polisi ikiongoza matenbezi hayo wakati yalipowasili katika barabara ya Haile Selassie Oysterbay leo asubuhi.
Rais
Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria kuanza kwa matembezi hayo kwenye
hoteli ya Golden Tulip kulia ni Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa
Vodacom Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw.
Wilbroad Slaa na kushoto kwa Rais ni Dk. Hadji Mponda wakishiriki
katika matembezi hayo leo asubuhi.
Rais Jakaya Kikwete akichukua mkasi kutoka kwa mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Grace Lyon tayari kwa kukata utepe.
Rais
Jakaya Kikwete wa pili kutoka kushoto pamoja na viongozi wengine
wakishiriki katika mazoezi kabla ya kuanza kwa matembezi hayo leo
asubuhi, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw.
Wilbroad Slaa .
Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania akitoa hotuba yake kabla ya kuanza kwa matembezi hayo leo asubuhi.
Watu mbalimbali waliojitokeza katika matembezi hayo wakiwa katika hoteli ya Golden Tulip leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw. Wilbroad Slaa akizungumza na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akizungumza na Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.
Wakiwa
katika mzungumzo kabla ya kuanza kwa matembezi hayo kulia ni Kamanda wa
Kanda Maalum ya Dar es salaam ya kipolizi Suleiman Kova, Mkuu wa Wilaya
ya Kinondoni Jordan Rugimbana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.
Hadji Mponda.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu Salva Rweyemamu akijadili jambo na Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa.
Comments