WAZIRI DK. EMMANUEL NCHIMBI AWAPATANISHA MBUNGE JOSEPH MBILINYI NA RUGE MUTAHABA WA CLOUDS MEDIA GROUP
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakipeana mikono leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa tofauti
zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka
miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa
Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia.
(Picha na Anna Nkinda - Maelezo)
Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia) akimsikiliza
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi wakati akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliotokana na sababu za kimuziki uliodumu kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akiongea
na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam
kuhusiana na kumalizika kwa mgogoro wa miaka miwili uliotokana na
sababu za kimuziki baina ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph
Mbilinyi (Katikati) na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba
(kulia). Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri Dk. Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.
Mbunge
wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa
Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakati akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam juu ya mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliodumu kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.
Comments