Na.Ashura mohamed ,Arusha
Wanachama
na wananchi wa mkoa wa Arusha wamepokea kwa masikitiko makubwa kitendo
cha timu yao kushuka daraja kutokana na malumbano ya viongozi yaliyopo.
Wanachama
hao ambao wameomba hifadhi ya majina yao walitoa malalamiko yao wakiwa
na uchungu mkubwa kwani kutokana na kushuka daraja kwa timu yao.
Walisema
kuwa wanaitupia lawama kubwa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Arusha
kwani ndicho kilichofanya hadi timu yao ikashuka.
"uanajua
tunalalamika kwanini tuliwaambia hawa viongozi wa wilaya watupe timu
yetu kama ikifa ifie mikoni mwetu wakagoma sasa wanaona walichokuwa
wanakita ka wamesababisha hadi timu yetu ikiashuka daraja "alisema
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hassani.
Nipashe
lilizungumza na baadhi ya wapenzi wa soka wa mkoa wa Arusha nao
walisema kuwa wamesikitishwa sana na kitendo cha timu hii kushuka
daraja kwani kwani walikuwa wanaitegemea kama ndio timu ya wananchi.
"kwakweli
tunasikitishwa sana kwa kitendo cha timu hiikushuka daraja kwani ndiho
timu tulikuwa tunaitegemea katika soka la mkoa wa Arusha sasa watu
wacheche wamesababisha hata timu yetu ikashuka tunalaani sana.
Nipashe
haikuishia hapo bali lilizungumza na mmoja wa waandishi wa habari
Mahmoud Ahmad alisema kuwa amesikitishwa sana kuona timu ambayo ilikuwa
ndio kioo cha michezo katika mkoa wa Arusha ikiachwa yatima hadi
kufikia kushuka daraja.
alitoa
ushauri kwa viongozi wa mkoa kuandaa timu mapema na kutafuta wafadhili
kwani wameona mechi tatu za timu ya Jkt Oljoro zikipotea kitu ambacho
sio jambo zuri na inaashirika kuporomoka kwa soka mkoani Arusha.
"viongozi
wasipoangalia kwa umakini tutabaki kuwa wasindikizaji katika soka hapa
nchini kitu ambacho ni aibu kubwa sana kwani awali katika mpira wa mkoa
huu kulikuwa na soka la zuri ambalolilimsisi mua kila mmoja lakini kwa
sasa limeondoka hamna soka kabisa tunaelekea kuwa watazamaji wa timu
zingine tu " alisema Mahamoud
Aidha
alitoa wito kwa viongozi ambao lawama kubwa zimetupiwa kwao kuwa
wajirekebishwe na watafute kazi zakufanya na sio kutegemea mpira jambo
ambalo linawafanya wakae kupigiana fitina katika soka na sio kusaidia
soka la mkoa wa Arusha
Kwa
upande wake katibu wa soka wa wilaya ya Arusha Zakayo Mjema alisema
kuwa yeye amepokea kwa masikitiko makubwa swala hili kwani wao kama
chama cha mpira walishirikiana kwa kila njia kuinusuru timu hii lakini
walishedwa.
Alisema kuwa
walitafuta ushirikiano kutoka kwa wanachama wa AFC lakini hawakupata
lakini kwa sasa timu hii imeshuka daraja wanatupiwa lawama kitu ambacho
sio cha haki .
Timu
hii ya AFC imekuwa ni timu ya kung'ang'aniwa na watu ambao wengi wao
wamekuwa wakiifanya timu hii shamba la bii hali iliyofanya kuifikisha
timu hii hapa ilipo na katika timu hii wachezaji wenyewe wamefanya kazi
ya ziada na kujituma vilivyo kwani kutokana na malumbano ya viongozi
hao na wanachama yalipelekea hata wacheza kwenda kucheza mechi bila
kula na wengine kuishi hata bila ya kupewa posho za kujikimu.Source full shangwe.
Comments