CAIRO, nchini Misri watu 74 wamefariki dunia na wengine 248 kujeruhiwa baada ya kutokea vurugu wakati wa mechi ya ligi kati ya timu zenye upinzani wa jadi za Al-Masry na Al-Ahly.
Vurugu hizo zilizuka katika mji wa Port Said wakati Al-Masry ilipokuwa ikiongoza kwa mabao 3-1, ushindi ambao umeelezwa kuwa ni wa kihistoria kwa timu hiyo dhidi ya wapinzani wao.
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Tottenham ya England, Hossam Ghaly alinusurika katika vurugu hizo. Ghaly, aliyeichezea Tottenham mechi 34 kati ya mwaka 2006 hadi 2009, ni nahodha wa Al-Ahly na alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 75.
Comments