Na Kijakazi Abdalla-Maelezo Zanzibar 15/02/2012
,Jaji
Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu amemteuwa Abdul-hakim Ameir Issa
kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumushi ya Mahkama Zanzibar
Akitoa
taarifa hiyo kwa Waandishi wa habari Mrajisi wa Mahakama Yessaya
Kayange amesema kuwa kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na Sheria ya
Utumishi wa umma namba 2 ya mwaka 2011 kifungu namba 34(2) ambapo
kifungu hicho kimemtaka Jaji wa mahakama kuteuwa mwenyekiti ambaye
anatakiwa kuwa na sifa za Jaji wa Mahakama kuu
Aidha
Jaji Mkuu ameteuwa wajumbe watano wa Tume hiyo , akiwemo Kadhi mkuu wa
Zanzibar Skh Khamis Haji Khamis , Safia Masuod Khamis Mwanasheria wa
Serikali anayemwakilisha Mwanasheria Mkuu, Salum Taufig Ali Wakili wa
kujitegemea anayewakilisha Chama cha Wanasheria Zanzibar , Othman
Bakari Othman Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Serikalini pamoja na
Hamidu A.S.Mbwezeleni ambaye ni Wakili wa kujitegemea pamoja na Yessaya
Kayange ambaye anakuwa Katibu wa Tume hiyo.
Pamoja
na hayo Mrajisi wa mahakama alisema kuwa kazi kubwa ya Tume hiyo ya
Utumishi ni kuajiri watu kushika nafasi za utumishi ikiwemo
kuthibitisha ajira zao za utuimishi
Akielezea
kazi za Tume hiyo Mrajis alisema kuwa ni pamoja na kushughulikia na
kupendekeza Serikalini mishahara na marupurupu ya watumishi wao pamoja
na kuidhinisha nyongeza ya utumishi mpaka miaka miwili.
Kazi
nyengine ya Tume hiyo ni kuthibitisha upandaji vyeo kwa wajiri pamoja
na kushughulikia suala lolote lililopelekwa kwake na Waziri, Katibu
Mkuu Kiongozi au Mkuu wa Taasisi kwa maamuzi au maelekezo.
Mnamo
tarehe 31.1.2012 Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makugu alizundua
rasmi Tume ya Utumushi ya Mahakama ili kuanza kufanya kazi zake ambapo
leo amewateua rasmi wajumbe wa Tume hiyo.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
Comments