Skip to main content

TAMKO LA VINEGA JUU YA MAKUBALIANO YA SUGU NA RUGE




Sisi kama kundi la Vinega kwa niaba ya umma wa watanzania wanaotuamini na kutusikiliza tumeridhia mapatano ya kumaliza ugomvi kati ya Mh. Joseph Mbilinyi (SUGU) na Bwana Rugemalila Mutahaba(ugomvi uliodumu kwa zaidi ya miaka 10 kabla hata ya anti-virus ikiwemo kutopiga nyimbo zake na kuporwa wazo la mradi wa malaria) ili kuweza kupiga hatua mpya katika kusaidia sanaa na pia kuonyesha dhamira yetu ya msingi kuwa, kwetu sisi ugomvi sio kati ya Sugu na Ruge bali ni mifumo mibovu ambayo imekuwa ikikumbatiwa na Bwana Ruge ili kuvuruga sanaa hii ya muziki na usambazaji, katika hili tutaweza kuwakomboa maelfu ya vijana wanaofanya muziki huu.
Sisi ni wawakilishi wa maelfu ya wafuasi wa mlengo huu ambao malengo husika yanafahamika, si rahisi sana kukaa meza moja na adui yako lakini kwa kuzingatia matakwa na maslahi ya wote na kufanikisha kile tulichokipigania(kwa hatua ya kwanza) mbele ya kamati ya Bunge na katika matoleo ya Anti virus yaliyopita tumejiridhisha kuwa malengo tuliyoyapigania na kuyaeleza kuwa hayapo sawa yamekubaliwa(kwa maana ya hoja zetu kushinda) na utekelezaji wake kufanyika mapema, kama ifuatavyo:-
• Studio iliyotolewa na Mh Rais kurudishwa na kukabidhiwa Chama halali cha kutetea wasanii (TUMA) kinachotambuliwa na BASATA .
• Chama feki cha wasanii TFU kuvunjwa na wasanii kuambiwa kujisajili na chama cha TUMA kwa utaratibu uliopo. (hakuna ubaguzi)
• Maboresho ya malipo kwa wasanii katika maonyesho. 
• Kuachwa mara moja kwa mizengwe iliyokuwa inafanywa na redio yao ya kutopiga nyimbo za wasanii mbalimbali kwa kigezo cha chuki na rushwa. 
Hayo ni baadhi ya mambo yaliyokubaliwa kutekelezwa na hatuoni kwanini tuendelee kukataa wito wa kumaliza suala hili na iwapo kama hawatatekeleza kama walivyosema hapo jamii itatuelewa kuwa sie sio wakorofi na tulikuwa na dhamira ya dhati katika kupata suluhisho la suala hili. 
Tunathamini juhudi zote za upatanishi wa suala hili uliofanywa na waheshimiwa wote katika hili ilikuleta tija na maelewano ya kweli tunataka haya yazingatiwe ili kutekeleza muafaka huu na kutimiza dhana ya dhati ya kusaidia sanaa yetu na wasanii wetu kwa ujumla wake. Tunaomba haya yafuatayo yazingatiwe na kuwekewa mkazo:- 
Pande hizi mbili zikutanishwe tena kwa nia ya kuweka mambo sawa kwa vyombo vya habari ili kuondoa ile hali ya sintofahamu ilijitokeza na kuchanganya wanajamii nchini kuwa, makubaliano hayo yaliyofanyika ni ya watu binafsi kati ya Sugu na Ruge (waliokuwa na ugomvi kwa zaidi ya miaka 10 sasa) na kamwe hayahusishi kundi la Vinega wa anti virus na redio nzima ya Clouds fm. - Bwana Rugemalila kutekeleza yale yote yalizungumziwa kuwa chanzo cha magomvi haya pamoja na kutoa suluhisho la tatizo la tuhuma za rushwa na upendeleo katika redio yao.Suala la mfanyakazi wao Othman Suka wa kitengo cha muziki kuwa kinara wa rushwa na upendeleo katika muziki pale redioni kwao pia lizingatiwe ili kupata muafaka wa kweli vinginevyo tatizo baso litaendelea kuwepo. -
Watangazaji wa Clouds Fm na menejimenti yao kuzingatia muafaka huu na kujiepusha na kauli zozote zitakazouweka muafaka huu katika hali ya mashaka, kauli za kejeli za Adam Mchomvu, DJ Fetty, B 12, Ncha kali na wenzake hakika zitauvunja muafaka huu na kurudisha suala hili lilipotoka. -
Utekelezaji ya yaliokubaliwa uende na wakati na katika hili dhamira ya kweli ya kutimiza haya ionekane. - Kila upande ukaamini kuwa haya yote yamefikiwa kwa ajili ya manufaa ya wasanii wote na si kwa maslahi ya wachache ili makubaliano ya kuivunja TFU na wasanii wote kujiungana TUMA chama cha wasanii kilichosajiliwa BASATA nail kufanyika mapema ili kupata mwanzo mpya katika sanaa yetu. - Tunaomba watanzania wenzetu waliotuunga mkono waone haya mapatanisho ni ushindi kwa vinega wote kwani tuliopigania yamekubaliwa utekelezaji pamoja na upungufu katika kutoa taarifa kwa mpangilio. Tunaomba watuunge tunavyoendelea na safari ngumu iliopo Mbele yetu. - Miongoni mwa malengo yetu ni kuhakikisha tunaondoa mfumo wote mbovu unounganisha watu wengi wakiwemo wakurugenzi/mameneja masoko wa makampuni kung’ang’ania kufanya kazi na radio moja na makampuni yake tu ili kuficha rushwa iliokithiri baina yao na kuwahimiza wapanue fursa kwa watanzania wote wenye uwezo wa kuandaa shughuli; kuhimiza redio na watumiaji wengine wa kazi za wasanii kulipa mirabaha watakayokubaliana kwa pamoja na TUMA kwa kutambua wasanii ndio chanzo cha mapato ya tasnia hii na wafanyabiashara wote katika sanaa waone ushirikiano na wasanii ndio njia ya kupata kipato kikubwa na kisicho na tafran, kuondoa woga wa wasanii kujiunga pamoja katika chombo chao ili kupata haki zao kama Vinega tulivothibitsha inawezekana na kuwasaidia wasanii watambue mchango mzuri wa redio na wafanyabiashara watakaofanya biashara nao kwa utaratibu utakaowekwa; Na kuendelea kuithibitishia Serikali na vyombo vyake vyote kama Bunge, TRA, Jeshi la Polisi, Mahakama nk ni manufaa kwao waamke na kufanya kazi ya dhati na TUMA na wadau wengine kuipanga hii “industry” ya SANAA ili kuboresha pato na maisha ya Watanzania.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...