Skip to main content

Mbowe: " Dr Slaa Ruksa Kugombea Arumeru"


ALIYEPEPERUSHA BENDERA CHADEMA 2010 AREJEA KUTOKA MAREKANI, AUNGA MKONO
Musa Juma na Moses Mashalla, Arusha
WAKATI Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akianza kugusa hisia za watu wanaomtaka agombee ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki, mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amesema iwapo mtendaji mkuu huyo wa chama ataamua kuwania kiti hicho, wataheshimu uamuzi wake.

Wakati Mbowe akitoa kauli hiyo, aliyepeperusha bendera ya Chadema katika uchaguzi wa mwaka 2010, Joshua Nasari na kutoa upinzani mkali kwa mgombea wa CCM, marehemu Jeremiah Sumari, naye amesema kama katibu mkuu wake ataamua kuwania kiti hicho, hatakuwa na pingamizi ikiwa chama kitaamua kwani lengo ni kutwaa jimbo hilo.

Akizungumza na Mwananchi jana baada ya kuibuka mjadala kuhusu uwezekano wa Dk Slaa kuwania jimbo hilo, Mbowe alisema, "Katika suala la kugombea, utashi binafsi ni jambo la msingi...,kama Dk Slaa ataamua kugombea ubunge  Arumeru Mashariki, tutaheshimu uamuzi wake."

Mbowe alisema katika uteuzi wa chama, kuna vigezo vinavyoangaliwa ikiwa ni pamoja na jinsi mtu anavyokubalika kwa wananchi anakogombea, sifa zake na utashi wake binafsi na kuongeza, "Hatuna uteule katika chama."

Hata hivyo, Mbowe alisema Chadema hakiwezi kumlazimisha Dk Slaa akagombee jimbo hilo kama mwenyewe utashi haumtumi kufanya hivyo, na kwamba hana shaka na kukubalika kwa katibu mkuu huyo kutokana na imani aliyojijengea kwa umma wa Watanzania.

Mbowe alisema Dk Slaa amekuwa akiombwa kugombea ubunge katika maeneo mengi likiwamo Jimbo la Igunga, lakini chama kisingeweza kumlazimisha kwani jambo la kwanza ilibidi mwenyewe aonyeshe utashi binafsi wa kutaka kuwania kiti hicho.

"Dk Slaa aliwahi kuombwa akagombee Igunga, lakini hakwenda. Hii ni kwasababu anakubalika nchini karibu kote, hivyo kama atakuwa na utashi binafsi kwanza, nadhani taratibu za chama zitatumika tu kufikia uamuzi," alifafanua.

Mwenyekiti huyo wa Chadema pia alitoa angalizo kwamba, wakati mwingine uamuzi wa chama kupata mgombea unaangalia jinsi mgombea alivyo na mtandao katika jimbo analotaka kugombea ili hata kama akichaguliwa aonekane ni mbunge wa eneo hilo.

"Ndiyo maana nasema kuna vigezo vingi tu, kwa mfano mtu anaweza kuwa mbunge mzuri bungeni, lakini je, ana connectivity (kinachomuunganisha) jimboni, kuangalia kama ana makazi na mtandao mwingine kwani asije akawa mbunge mzuri bungeni, lakini jimboni akiwa kama mgeni hivyo watu wakaona kama kimewapelekea pandikizi tu,"alifafanua Mbowe.

Tangu juzi kumekuwa na mjadala katika mitandao ya kijamii huku baadhi wakimtaka Dk Slaa akagombee ubunge Arumeru Mashariki kuziba pengo la aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Marehebu Sumari, lakini wengine wanapinga na kumtaka aendelee kubaki na nafasi yake ya katibu mkuu wa chama kwa lengo la kukijenga.

Hata hivyo, Dk Slaa ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 alishika nafasi ya pili akiwa nyuma ya Rais ya Jakaya Kikwete, juzi alinukuliwa na gazeti moja la kila siku (siyo Mwananchi) akisema, "Siwezi kulizungumzia jambo hilo, maana nilikwisha kusema muda mrefu kuwa sitaki tena ubunge na isitoshe mimi si mwenyeji wa Arumeru,"

Joshua Nasari
Kwa upande wake Nasari (26) ambaye ana mtaji mkubwa wa kura kufuatia matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2010 alitoa msimamo wake akisema  yupo tayari kufanya mazungumzo na viongozi wa juu ya chama chake juu ya kumpisha Dk Slaa kuwania ubunge katika jimbo hilo kama akihitaji.
 
Nasari ambaye amerejea hivi karibuni mjini Arusha akitokea nchini Marekani, leo anatarajiwa kuchukua fomu rasmi ili kuwania nafasi hiyo kupitia Chadema.

"Nimesikia maoni kupitia mitandao na wadau wakimuomba Dk Slaa kugombea, hili ni jambo jema kwetu kwani wananchi wanajua jimbo hili tunashinda Chadema na kama Dk (Slaa) akitaka kugombea dekomrasia ya chama chetu itafanya kazi, kwani kikubwa tunataka ushindi,"alisema Nasari.

Nasari aliyewahi kuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) kati ya 2008 na 2009 alipohitimu shahada ya Sayansi ya Jamii katika masuala ya utengenezaji Sera na Utawala, alisema ana imani Chadema kitashinda Arumeru.
 
"Nilikuwa Marekani kikazi na sasa nimerejea kama ulivyoshuhudia watu wengi wananiunga mkono na tayari wamenichangia Sh 11milioni za kampeni na magari manane," alisema Nasari.
 
Mgombea huyo ambaye tayari ametangaza kuacha kazi katika shirika la Kimarekani la Foundation For Tomorrow  ili kujikita kwenye uchaguzi huo, alisema wakazi wa Arumeru Mashariki wanahitaji mwakilishi sahihi ambaye anaweza kuwatetea katika kuinua uchumi wao.
 
Hata hivyo, alisema tayari amepata taarifa za Dk Slaa kutoa tamko kuwa hawezi kushiriki katika uchaguzi huo, kwa kuzingatia kuwa sio mkazi wa Meru na pia hana nia ya kugombea kiti hicho.
 
"Nategemea Dk Slaa na viongozi wengine wa kitaifa, wakiwapo wabunge, marafiki zangu wa vyuo vikuu na wengine wengi tutakuwa nao Arumeru kuhakikisha Chadema inashinda,"alisema Nasari.
 
Hadi  kufikia jana, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Mkoa wa Arusha (Bavicha),  Ephata Nanyaro,  wanachama waliokuwa wamechukua fomu ni Yohane Kimuto, Samweli Chami na Rebecca Mwingisha na leo Nasari atakuwa mwanachama wa tatu.
 
"Tunatarajia wanachadema wengi zaidi watajitokeza katika siku hizi zilizobaki ili kuchukuwa fomu na kurejesha mapema,"alisema Nanyaro.
 
Mgombea CCM alalamikia rushwa
Katika hatua nyingine, Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM katika Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Elirehema Kaaya ambaye pia ni afisa wa mifugo mkoani Mwanza, amekitaka chama hicho kukemea kampeni za fedha ndani ya chama katika uchaguzi huo.
 
Kaaya ambaye pia aligombea jimbo hilo katika uchaguzi uliopita na kushindwa katika kura za maoni ndani ya CCM, alisema wakazi wa Arumeru hawahitaji mgombea wa CCM ambaye anapata nafasi hiyo kwa kutumia fedha.
 
"Arumeru wanataka mtu wa kuwasemea matatizo yao mjengoni (bungeni) na sio mtu anayetumia fedha kupata ubunge na mimi naomba chama kikemee na kukomesha matumizi ya fedha,"alisema Kaaya.
 
Akizungumzia maombi hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Arumeru Edson  Lihweuli alionya mgombea yoyote ambaye atabainika kujihusisha na vitendo vya rushwa au kukiuka taratibu atachukuliwa hatua.
 
Lihweuli alisema.... Soma zaidi: http://www.mwananchi.co.tz

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was

HAYA NI MAKAO MAKUU YA MTANDAO WA Tigo TANZANIA DAR ES SALAAM

MAHALA yalipo ni Lugoda Street Gerezani Industrial Area , kwa sasa mdandao huu umefanya makubwa , kuna Tigo Bwerere Uilisha cheki hiyoooooo watu full kujiachia wana chonga tuu kwenye vyao vilonga.