Mara Baada ya magazeti
mengi ya udaku jana nchini kuandika kwamba lile kundi la vichekesho
nchini Original Komedi,ambalo linaonyesha vichekesho vyako kwenye
runinga ya Taifa Tbc 1,kwamba limesambaratika ni uzushi mtupu...Kwa
mujibu wa kiongozi na muasisi wa kundi hilo Sekion David amesema “Hayo
ni maneno ya uzushi ya watu, mambo yetu sisi huwa hatupendi
kuyazungumza hadharani, watu wako likizo baada ya muda watarudi hewani,
ukienda kwenye website yetu huwa tunaandika kila kinachoendelea, hizo
taarifa hazina ukweli wowote”Hata hivyo kwenye website yao, kuna
tangazo linasema Orijino Komedi na timu nzima itakua likizo kwa mwezi
january 2012 tu, baada ya hapo watarudi kazini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu

Comments