Wachezaji
wa timu ya Yanga wakishangilia mbele ya mashabiki wao mara baada ya
mchezaji wa timu hiyo Khamis Kiiza, kuifungia timu hiyo goli la
kuongoza katika kipindi cha kwanza,Tayari mpira umekwisha na timu ya
Zamalek imefanikiwa kusawazisha goli na kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka
mwisho wa mchezo.
Huu ni mchezo wa mashindano ya Klabu
bingwa barani Africa yanayoandaliwa na shirikisho la vyama vya mpira wa
miguu (CAF), timu hizo zitarudiana tena nchini Misri baada ya wiki
mbili zijazo.
Mmoja
wa wachezaji wa Yanga akipiga mpira kuelekea lango la Zamalek huku
mlinda mlango wa timu hiyo akijaribu kuzuia ili mpira huo usilete
madhara katika lango lake.
Comments