Katika
mkutano wa mawaziri wa Fedha wa mataifa tajiri kabisa, G-20, unaofanywa
mjini Mexico City, Waziri wa Fedha wa Brazil, Guido
Mantega, alisema nchi chipukizi zitatoa fedha zaidi kusaidia kupunguza deni la mataifa ya Ulaya.Lakini nao badala yake, wanataka kupewa madaraka zaidi katika Shirika la Fedha Duniani, yaani IMF.
Waziri wa Fedha wa Brazil ameingia mkutanoni na ujumbe wazi : kwamba nchi chipukizi ziko tayari kuzisaidia nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya Euro, na ambazo zimekabwa na madeni, lakini msaada wenyewe utakuwa wa shuruti.
Guido Mantega alisema nchi kama Mexico, India na Brazil zitasaidia, lakini kuna shuruti mbili.
Kwanza Ulaya yenyewe izidishe akiba katika kasha au sanduku la fedha ili kujisaidia panapo dharura.
Kuna hisia katika G-20 kuwa siyo lazima kwa nchi nyengine kulisaidia eneo la Euro, hadi Ulaya yenyewe inaweka akiba zaidi kujisaidia.
Shuruti ya pili alisema Bwana Mantega ni kwamba mabadiliko yaliyoahidiwa, kuwa mataifa chipukizi nayo yatawakilishwa zaidi kwenye bodi ya uongozi wa IMF, yatekelezwe.
Ahadi hiyo ilitolewa wakati Brazil, Urusi, India na Uchina zilipozidisha mchango wao katika mfuko wa akiba ya dharura wa IMF, mwaka wa 2008.
Hadi sasa marekibisho hayo hakufwatliwa, na hasa nchi za Ulaya, zinang'ang'ania viti vyao katika bodi ya uongozi ya IMF.
Comments