Release No. 031
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 27, 2012
MAKOCHA POULSEN (TAIFA STARS), ANGELS (MAMBAS)
Makocha
Jan Poulsen wa Tanzania (Taifa Stars) na Gert Josef Angels wa Msumbiji
(Mambas) kesho (Februari 28 mwaka huu) watakuwa na mkutano na waandishi
wa habari kuzungumzia maandalizi ya timu zao.
Taifa
Stars na Mambas zitapambana Februari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam kuanzia saa 10 jioni katika mechi ya kwanza ya mchujo kuwania
tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON)
zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Mkutano
huo na waandishi wa habari ambapo makocha hao pia watajibu maswali ya
waandishi wa habari utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ukumbi wa
mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Mambas
iliwasili nchini jana (Februari 26 mwaka huu) ikiwa na wachezaji 19 na
viongozi kumi. Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho ni Francisco
Muchanga, Clesio Bauque, Almiro Lobo, Manuel Fernandes na Francisco
Massinga.
Wengine
ni Joao Rafael, Nelson Longomate, Joao Mazive, Zainadine Chavango,
Osvaldo Sunde, Luis Vaz, Carlos Chimomole, Joao Aguiar, Edson Sitoe,
Jeremias Sitoe, Stelio Ernesto, Elias Pelembe, Eduardo Jumisse na Simao
Mate.
MECHI YA YANGA, ZAMALEK KUCHEZWA SAA 12
Mechi
ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Zamalek na Yanga
itachezwa Machi 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jeshi jijini Cairo kuanzia
saa 12 jioni kwa saa za Misri.
Kwa
mujibu wa maelekezo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) mechi
hiyo itachezwa bila washabiki kwa vile Zamalek inakabiliwa na adhabu ya
kucheza mechi hiyo bila washabiki.
Mechi
hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco ambao ni Jihed Redouane,
Rouani Bouazza na Bekkali Mimoun wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Gihed
Greisha wa Misri. Kamishna wa mchezo huo ni Ben Khadiga wa Tunisia.
WASOMALI KUCHEZESHA SIMBA, KIYOVU
Mwamuzi
i Yabarow Hagi Wiish na wasaidizi wake Aweis Ahmed Nur na Abdirahman
Omar Abdi, wote kutoka Somalia ndiyo watakaochezesha mechi ya marudiano
ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Kiyovu Sport ya Rwanda.
Kwa
mujibu wa orodha ya waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF), mwamuzi wa akiba kati mechi hiyo namba 14 itakayochezwa Machi 4
mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam atakuwa Waziri Sheha wa
Tanzania. Kamishna wa mechi hiyo ya raundi ya awali atakuwa Jean Marie
V. Hicuburundi kutoka Burundi.
CAF
imeziingiza moja kwa moja kati raundi ya kwanza timu 16 kutokana na
ubora wake. Timu hizo ni ES Setif (Algeria), Interclube (Angola), Asec
Mimosas (Ivory Coast), Enppi (Misri), AS Real Bamako (Mali), CO de
Bamako (Mali) na CO Meknes (Morocco).
Nyingine
ni WAC (Morocco), Warri Wolves (Nigeria), Heartland (Nigeria), St. Eloi
Lupopo (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Us Tshinkunku (Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Amal Otbara (Sudan), Al Ahly Shandy
(Sudan), CSS (Tunisia) na CA (Tunisia).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Comments