Skip to main content

WABUNGE WAKUTANA NA WATAALAM WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012



  Waziri wa Fedha Mustapha Mkulo akitoa maelezo ya awali kuhusu maendeleo ya kazi za maadalizi ya sensa ya watu na makazi iliyopangwa kufanyika nchini wakati wa semina  kati ya wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Jamii na Kamati  ya Fedha na Uchumi  iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma,Hata hivyo waziri Mkulo amefafanua kuwa serikali itahakikisha kuwa sensa hiyo inafanyika kama ilivyopangwa kwa ubora na ufanisi ikilinganisha na sensa zilizopita.
 Manaibu waziri wa Fedha Gregory Theu (kushoto) na Pereira Silima(kulia) wakifuatilia masuala mbalimbali kuhusu Sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka huu wakati semina  iliyowahusisha wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Jamii na Kamati  ya Fedha na Uchumi  jana mjini Dodoma.
  Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Jamii na Kamati  ya Fedha na Uchumi wakifuatilia taarifa mbalimbali kuhusu maandalizi ya sense ya watu na makazi itakayofanyika mwaka walipokutana na wataalam kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu jana mjini Dodoma.
Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Sensa Dkt. Albina Chuwa akisisitiza jambo kwa wajumbe  wa kamati ya Maendeleo ya Jamii na Kamati  ya Fedha na Uchumi  kuhusu zoezi la sensa ya watu litakalofanyika  nchi nzima mwezi Agosti mwaka huu jana mjini Dodoma.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Comments