Waandishi wetu
WAKATI tetesi za kupanguliwa Baraza la Mawaziri zikizidi kupamba moto, hali ya afya ya baadhi ya mawaziri imeelezwa kuwa tete hivyo kulazimika kupelekwa India kwa matibabu.Miongoni mwa Mawaziri hao ni wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami ambaye jana aliibuka na kuwataka watu aliowaita wanye uchu wa kuchukua nafasi yake, waache mara moja kutumia afya yake kupiga propaganda chafu za kisiasa. Hadi sasa, mawaziri ambao taarifa za kuugua kwao zinafahamika ni pamoja na Profesa Mark Mwandosya mwenye dhamana ya Maji, Naibu Waziri Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na Dk Chami. Wengine ambao taarifa zinaonyesha kuwa walikuwa nje ya nchi kwa matibabu ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe na Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani. Ingawa haijafahamika maradhi yanayowasumbua hadi sasa, wadadisi wa mambo ya kisiasa wamekuwa wakichukulia hali ya afya ya baadhi yao kama moja ya sababu inayoweza kuwafanya wawekwe kando pale Rais Jakaya Kikwete atakapoamua kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ili kuwapa fursa ya kupumzika na kuendelea na matibabu. Dk Chami Dk Chami alisema jana kwamba tangu arejee kutoka India alikokwenda kutibiwa, afya yake imeimarika na hakuna siku aliyoshindwa kutekeleza majukumu yake huku akisema wanaoeneza uvumi huo ni mahasimu wake kisiasa wanaonyemelea nafasi yake. Alisema mbali ya kufika ofisini kwake kila siku, alishiriki kikamilifu kwenye Mkutano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano uliomalizika hivi karibuni Mjini Dodoma na kujibu hoja mbalimbali zilizoelekezwa kwa wizara yake. Aliwalinganisha maadui zake kisiasa na fisi mwenye uchu anayemfuatilia mtu kwa nyuma bila kujali umbali wa safari kwa matumaini ya kuneemeka mkono ukidondoka huku akisema Rais Jakaya Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya kuteua mawaziri wake kwa vigezo anavyoona vinafaa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo. “Nashangaa sana, afya yangu ni njema, imeimarika. Tangu nimerejea kutoka India, sijawahi kwenda hospitali wala zahanati yoyote, naingia ofisini kila siku kuanzia asubuhi na kutoka jioni, nimehudhuria Mkutano wa Bunge, Dodoma na leo nina kazi ya kutembelea viwanda, sasa huku ndiko afya yangu kuzidi kudorora?,” alihoji Dk Chami na kuongeza: “Suala kubwa hapa ni uwaziri, lakini.... Soma zaidi; http://www.mwanachi.co.tz |
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments