Artist wa bongo movie, Baby Mahada amefunguka kuwa malengo yake aliyojiwekea ni kuja kugombea ubunge kwa siku za usoni.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, msanii huyo alisema kuwa hashindwi kuwatumikia wananchi hivyo baada ya miaka kadhaa ataingia katika vinyang'anyiro vya viti vya ubunge.
Alisema kuwa sababu kubwa inayomfanya kutaka kuchukua maamuzi hayo ni kutokana na vitendo vya baadhi wanasiasa kutowajali wananchi ambao ndiyo waliyowapa dhamana.
“Malengo yangu ni kuja kuwa mbunge na kikubwa ambacho nataka kukifanya ni kuwatumikia Watanzania, ambao kila siku wanalia juu ya wasansiasa ambao wanafanya kazi hiyo kwa ajili ya maisha yao binafsi,” alisema.
Comments