Victor Costa ambaye ni beki wa wekundu wa msimbazi timu ya Simba amerejeshwa kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya uongozi kuamua kumsamehe.
Costa alisimamishwa kuichezea timu hiyo kwa muda usiojulikana kwa makosa ya tuhuma za utovu wa nidhamu.
Beki huyo wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars, anadaiwa kutenda vitendo hivyo wakati timu hiyo ilipokwenda Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, tayari beki huyo ameshaanza mazoezi na wenzake.

Comments