Skip to main content

MKUTANO WA SITA WA BUNGE KUHITIMISHWA LEO.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda akiingia ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini kuongoza kikao cha tisa cha mkutano wa sita wabunge ambapo bunge linahitimisha shughuli zake mjini Dodoma.
Mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango akijadili jambo na Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Frederick Werema ndani ya ukumbi wa Bunge leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu mjini dodoma


Mbunge wa Singida mjini Mohammed Dewji akimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais  Uhusiano na Uratibu Stephen Wasira ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.
 
Wajumbe na Viongozi wa chama cha wamiliki wa shule  Vyuo na shule binafsi (TAMONGSCO) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoka ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma. Viongozi hao wapo bungeni Dodoma  kukutana na kamati ya kudumu  ya bunge ya huduma za jamii kwa lengo la kuhimiza ushirikiano kati yao na wabunge pamoja  na serikali ili kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto zinazoikabili sekta binafsi ya elimu nchini Tanzania.
 Mbunge wa Bumbuli January Makamba akiwasilisha Hoja binafsi kuhusu sheria ya udhibiti wa shughuli za upangaji nyumba za makazi aliyoitoa chini ya kanuni ya 54 (1) ya kanuni za bunge toleo la 2007 ya kuliomba bunge kuazimia kwa kauli moja ,kuitaka serikali katika mkutano ujao wa saba kuleta Muswaada wa Sheria ya kudhibiti Upangaji wa Nyumba na Makazi kufuatia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wanaoishi mijini kutokana na adha wanazopata katika kutafuta nyumba za kupanga au kuishi kwenye nyumba hizo. 
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiwasalimia viongozi na wachezaji wa timu ya Villa Squard ya Kinondoni jijini Dar es salaam waliofika bungeni hapo kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na bunge. 
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya sekondari Hijra ya mjini Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge Dodoma.
  
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Comments