Mshambuliaji wa klabu ya Borrussia Dortmund ya Ujerumani raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang leo ametia saini mkataba wa muda mrefu kuichezea klabu ya Arsenal. The Gunners waliwasilisha maombi mawili ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ambayo yalikataliwa na Dortmund kabla ya kukubali dau la juu ya £46.5m walilomsajilia Alexandre Lacazette. Klabu ya Arsenal imeandika kwenye mtandao wao kwamba Aubameyang ni Mchezaji wao wa pili kumnunua katika kipindi cha kuhama wachezaji mwezi Januari.