Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2013

HILI NDIYO JENEZA ATAKALO SAFIRISHWA NALO MAN NGWEA KWA NDEGE KUTOKA AFRIKA KUSINI HADI BONGO

Nje ya mochwari ya Serikali Hillbrow Johannesburg ulikohamishiwa mwili wa Ngwea.Picha za chini  ni Watanzania wakiongozwa na Kinje Ngomale Mwiru wakitazama sample ya majeneza mbalimbali ili wajue la kununua, hapa walikua na mfanyabiashara wa kampuni ambayo pia huwa inashughulika na kusafirisha miili ambapo gharama yake ni zaidi ya milioni nne na nusu Wakikagua sample ya jeneza  Watanzania wa ishio Afri k a ya Kusini walipoku tana juu ya msiba wa Albert Mangwea. Kifo cha Ngwear kimetokea juzi nchini humo baada ya kukutwa chumbani kwake akiwa tayari amefariki na msanii mwenzaki M to the P akiwa hajitambui.   Millard Ayo akifanya interview na promota Mtanzania ambae alikua tayari na kazi ya show tatu za ziada ya Ngwea kabla hajafariki, zilipangwa kufanyika siku kadhaa zijazo.…  Mwili wa marehemu N gwair bado upo mochwari ya Serikali Hillbrow Johannesburg na leo ndio unafanyiwa uchunguzi ili kujua nini sababu za kifo chake.Pia...

Tumia macho hapa !

 Si za bandia bali zimefugwa, na ni takribani miaka mitatu sasa hazijakatwa.

KAMA ZAMANI !

Ngaoma hii imetulia , FA umekuwa  na kawaida ya kutisha katika 'gemu' la Hip Hop Bongo . Big Up.

R.I.P Jembe

ALIVYOFUNGUKA DIAMOND :NAMPENDA PENNY KULIKO WEMA

  MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul 'Diamond' amekiri kuwa anampenda zaidi mpenzi wake mpya, Penny Mungilwa kuliko ilivyokuwa kwa mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu. Diamond alisema mjini Dar es Salaam wiki hii kuwa, mapenzi yake kwa Penny yamemfanya ajione kama vile ameoza kwa binti huyo. "Ni sawa na kusema treni imegonga mwamba maana kila ninapokuwa naye, nasikia raha ya ajabu, sijui ameniroga. Ananipenda mno,nami nampenda, kwake nimefika,"alisema Diamond. Msanii huyo nyota wa bongo fleva alisema japokuwa udanganyifu katika mapenzi ni jambo la kawaida, lakini Penny hajawahi kuonyesha dalili hiyo kwake. Alisema kwa kawaida, mwanamke anapofanya udanganyifu wa mapenzi, inakuwa aibu kwa mwanaume, lakini udanganyifu huo ukifanywa na mwanaume, inakuwa sifa kwake. "Ni kweli Wema alinipenda, alinionyesha mapenzi ya dhati, lakini alifanya udanganyifu hadharani, alinivunjia heshima, alinivunja moyo, sikupenda k...

Nyota wa Kibao cha CALL BOX Ajutia wimbo wake huo!

MWANAMUZIKI nyota nchini, Muumin Mwinjuma amesema hakuna kitu anachokijutia katika maisha yake kimuziki kama kutunga wimbo wa Call Box. Akizungumza mjini Dar es Salaam wiki hii, Muumin alisema wimbo huo ulipoteza heshima yake kimuziki na kumfanya achukiwe na wanawake wengi kwa kuhisi alimtungia mkewe wa pili. Muumin alisema hadi sasa bado anakuna kichwa ili kurejesha heshima yake kimuziki, hasa kwa wanawake, ambao alikiri kuwa ndiyo mashabiki wake wakubwa. Alikanusha madai kuwa, alitunga wimbo huo kwa lengo la kusimulia mkasa uliomfanya aachane na mkewe wa pili baada ya kumfumania mara mbili. "Huu wimbo nilipewa na rafiki yangu mmoja, ambaye ni mganga wa kienyeji, aliniomba niuimbe. Bahati mbaya sana, nilirekodi wimbo huu muda mfupi baada ya kuachana na mke wangu, ndio sababu mashabiki wengi walidhani nimemwimbia yeye,"alisema. Muumin alisema mashabiki wake wengi ni wanawake kutokana na kuzipokea vizuri nyimbo zake za Mgumba namba moja na namba mb...

Saudi Arabia yatoa msaada wa dola milioni 24 kwa Somalia

Na Abdi Said, Mogadishu Kampeni ya Kitaifa ya Saudia kwa Kuwasaidia Watu wa Somalia imeahidi kutoa mfuko wa msaada wa kina wenye thamani ya dola milioni 24 kwa miradi ya ujenzi mpya nchini Somalia, kwa mujibu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), ambao unasaidia kuratibu fedha hizo. Mwanamke wa Somalia akitembea karibu na kambi ya watu wa ndani waliokimbia makazi yao mjini Mogadishu tarehe 3 Mei. Sehemu ya msaada wa Saudia ulioahidiwa Somalia utatumiwa kuwapa makazi watu waliokimbia makazi yao. [Na Tobin Jones/AU-UN IST/AFP] Msaada huo utakwenda kwa mikoa yote ya Somalia na utaelekezwa katika sekta za elimu, afya, kilimo pamoja na kuwarekebisha watu waliokimbia makazi yao na katika hali zote za ustawi wa jamii, OIC ilisema katika taarifa hapo tarehe 12 Mei. Wigo wa mfuko wa misaada na ushirikishwaji wa asasi zisizokuwa za kiserikali, wazee wa kikabila, tawala za mikoa na serikali ya shirikisho katika kuamua miradi gani ya kutekeleza inaashiri...

Wenye divisheni ziro 30,000 wapeta

Dar es Salaam. Wanafunzi 30,063 waliopata daraja sifuri katika matokeo yaliyopita, wameula baada ya kupandishwa hadi daraja la nne kutokana na ukokotoaji upya wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyofanywa na Baraza la Mitihani la Taifa (Nacte) na kutangazwa jana. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa Marekebisho hayo yalifanyika baada ya kufutwa kwa matokeo ya awali yaliyotangazwa Februari 18, mwaka huu. Kufutwa kwa matokeo hayo, ilikuwa ni utekelezaji wa sehemu ya mapendekezo ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, baada ya wanafunzi 240,909 kupata daraja sifuri kwenye matokeo yaliyotangazwa mara ya kwanza. Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema sasa watakaokuwa na sifuri ni 210,846 sawa na asilimia 56.92 wakati wavulana wakiwa ni 104,259 na wasichana 106,587. Hiyo ina maana kuwa sasa ufaulu umepanda na kuwa asilimia 43.08 badala ya ule wa kwanza ambao ulik...

Meneja wa CRDB ahukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa wizi

Na Happiness Katabazi, Mwanza -- MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mwanza, imemhukumu kifungo cha miaka mitano jela Meneja wa Benki ya CRDB wa matawi ya Nyanza na Bugando mkoani Mwanza, Daniel Peter Waijaha, pamoja na mteja wa benki hiyo, Dismas Mohamed Ndaliko baada ya kuwakuta na hatia wa kosa la wizi wa jumla ya Sh Milioni 140 mali ya benki hiyo. Read more...

Magazeti ya Leo

Rest in Peace Jembe

Habari zilizonifikia jana   ni kwamba msanii wa maarufu wa  Bongo flava Albert Mangweair pichani amefariki dunia jana.

Flaviana Matata!

      Huyo ni mwanamitindo wa nchini anaye fanya vizuri anga za mitindo kimataifa.

HIKI NDICHO KILICHOMUUA NGWEA

Habari kutoka kwa mtu wa karibu na Rapper Ngwea, aliejitambulisha kwa jina la Hamisi, amesema Ngwea alikua kule kwa mualiko wa kufanya show South Africa, ambapo alikua na msanii mwingine anaeitwa M to the P, na walitakiwa kuondoka leo kurudi Dar saa tatu asubuhi, lakini baada ya kuona hawatokei ndio wakaamua kwenda walipokuwa wamefikia na kuwakuta wote wawili wakiwa hawajielewi baada ya kujidunga madawa ya kulevya mengi (overdose), walipowahishwa hospitali, habari ndio ikawa hivi, kuwa Ngwea amefariki na M to the P yuko hoi hospitali May God give you peace brother.Blog ya Dj Fetty jana iliandika hivi.

EMMANUEL NCHIMBI: Tanzania Ni Salama

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema itahakikisha inaendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa Watanzania na raia wa kigeni waliopo na wanaoendelea kutembelea hapa nchini kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za binafsi na kimaendeleo ili watu wote waweze kutekeleza majukumu yao na kuishi kwa amani na usalama nchini. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alisema hayo jana wakati akizungumza katika kikao baina yake na Ujumbe wa Wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya na mabalozi wa nchi hizo hapa nchini kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo. Taarifa ya wizara ilisema Nchimbi alisema kwa sasa Serikali kupitia polisi imejiwekea mikakati mbalimbali ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla. ‘‘ Polisi tayari imeanzisha dawati maalumu litakalowahudu...

Kliniki za afya za AMISOM zawatibu Wasomali katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-Shabaab

Na Abdi Said, Mogadishu Katika kipindi cha miezi sita iliyopita, Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) imefungua kliniki za afya nane na hospitali tatu katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-Shabaab, kwa mujibu wa msemaji wa AMISOM Kanali Ali Aden Humad. Wakina mama na watoto wakisubiri huduma za matibabu kwenye kituo cha jeshi cha AMISOM huko Halane jijini Mogadishu. [Abdi Said/Sabahi] Kliniki hizo zipo katika wilaya kadhaa za mikoa ya Shabelle ya Kati na ya Chini, na hospitali hizo zipo Beledweyne, Kismayo na Baidoa. Zinatoa huduma kamili mbalimbali za afya, Humad alisema. "Tuna vifaa vya kisasa vya huduma za afya, ikiwa ni pamoja na vifaa vya maabara kwa ajili ya kuchunguza magonjwa ya kawaida, mashine ya kufanya eksirei kwa jeraha ya mfupa, mashine ya kuchunguza shinikizo juu la damu na kisukari, na dawa hutolewa bure na madaktari wenye sifa za hali ya juu," aliiambia Sabahi. AMISOM imeweka katika hospitali hizo ...

Urusi: Lazima nchi ya Iran ijumuishwe kwenye mazungumzo ya amani nchini Syria

Na Emmanuel Richard Makundi Nchi ya Urusi imesema ni lazima Serikali ya Iran ihusishwe kwenye mazungumzo ya kusaka aamani ya Syria kama kiungo muhimu na mshirika wa karibu wa utawala wa rais Bashar al-Assad. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry (kushoto) akiteta na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov (kulia)  Photograph: Sergei Ilnitsky/EPA Kauli ya Urusi inamaanisha kupuuzilia mbali maombi ya baadhi ya mataifa ya magharibi ambayo yametaka kujumuishwa kwenye mkutano wa kimataifa wa mjini Geneva, mkutano unaolenga kusaka amani ya kudumu nchini Syria. Lakini kauli ya sasa ya Urusi kutaka nchi ya Iran nayo iingie kwenye mazungumzo ya kusaidia kupatikana kwa amani ya kudumu nchini Syria imekosolewa na nchi za magharibi ambazo zinaiona Iran kama mfadhili mkuu wa silaha kwa wapiganaji wa Hezbollah wanaousaidia utawala wa Assad. Hapo jana waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesisitiza nchi yake kutuma silaha zaidi za kijeshi kw...

Wawakilishi wa Tanzania kwenye ‘Big Brother Africa 2013 - The Chase’

Shindano la Big Brother Africa 2013 limezinduliwa rasmi leo ambapo Show yake iliruka rasmi na kuwapa fursa mashabiki mbalimbali kujua nchi zao zinawakilishwa na washiriki gani. Kutoka Tanzania, tunawakilishwa na Nando pamoja na Feza Kessy. Nando ni mwanafunzi (Mtanzania) ambaye inasemekana anaishi USA, Los Angeles na alikopa nauli ili aje Tanzania kwa ajili tuu ya kushiriki kwenye Auditions za BBA, na amefanikiwa. [See More] »

MAAFISA 30WA JESHI LA MAGEREZA WAVISHWA NISHANI

Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja akikagua Guard ya Heshima iliyoandaliwa kwa ajili yake kabla ya kuanza zoezi la Uvalisha Nishani kwa Maafisa na Askari wa Magereza toka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini  katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga, Moshi, Kilimanjaro Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (kulia) akimvalisha Nishani ya Utumishi Uliotukuka Kazini, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Hamis Nkubasi. Jumla ya Maafisa na Askari 30 kutoka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini wamevalishwa Nishani mbalimbali. Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali, John Minja (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa Nishani mara baada ya zoezi la Uvalishaji Nishani kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini l katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga...

FASHION WEEK

FASHION WEEK First-ever event celebrating local and locally inspired fashion design in Zanzibar set to premiere in October. This October, the all-new Fashion Week Zanzibar will take over Stone Town’s prolific Mtoni Palace in a celebration of local fashion and unique East African design. The new initiative is dedicated to showcasing fashion created in or inspired by the beautiful island of Zanzibar, Tanzania. The island’s homegrown fashion industry has been developing in exciting new ways in recent years. One-of-a-kind designs pulling from the varied influences of Zanzibari culture and island life, mixed with the brightly coloured patterns of kanga and kitenge, create a strong sense of place and culture in the local fashion industry. The event is founded and organized by photographer and businessman Javed Jafferji, internationally renowned designer Farouque Abdela, and budding photographer Adnan Abbas. “We decided to celebrate Zanzibar’s up-and-coming fashion a...

WARSHA YA UTENGENEZAJI FILAMU- MAOMBI YAFUNGULIWA

ZIFF sasa inapokea maombi kutoka kwa watengenezaji filamu Afrika Mashariki wanaotaka kushiriki katika warsha ya utengenezaji filamu wakati wa ZIFF mwaka huu.. Wanafunzi 5 (mmoja toka kila nchi ya Afrika Mashariki) watalipiwa safari, malazi na chakula ili kushiriki kwenye warsha hiyo. Wanafunzi 5 wengine watajilipia wenyewe. Mfumo wa warsha utakuwa ni kufuatilia kikundi cha watengeneza filamu walio tayari mafundi watakaokuwa wanatengeneza filamu fupi wakati wa ZIFF. Utengenezaji huu unaitwa Guerilla Filmmaking (yaani filamu chapchap) na katika siku 6 filamu itapigwa, itahaririwa na kuonyeshwa ZIFF siku ya mwisho. Wanaotaka kushiriki kwenye warsha watume maombi yao hivi: CV fupi. Maelezo kwa nini wachaguliwe (maneno 1000) Maombi yatumwe kwa: workshop@ziff.or.tz Warsha imedhaminiwa na Goethe Institute na GIZ (Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani) na Jumuia ya Africa Mashariki (EAC) Maelezo pia yako www.ziff.or.tz

ka kobe:Maafande na utulivu Ntwara

Waunda timu ya urais Uchaguzi Mkuu wa 2015

Mwanza. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema wakati ukifika, yeye na rafiki zake Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, watachagua mmoja wao watakayeona anafaa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. Samweli sitta Waziri Sitta aliyasema hayo jana katika Kongamamo la Mawasiliano katika Nyanja za Digitali la wanafunzi wa Idara ya Uhusiano na Masoko, Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT), Mwanza. Mara ya kwanza, Sitta aliwataja rafiki zake hao juzi wakati wa harambee ya kuchangia Kanisa Katoliki, Josephine Bakita, Parokia ya Igoma, Mwanza. Pia alisema hatagombea tena Ubunge Urambo ya Mashariki baada ya kuwa katika ulingo wa siasa kwa miaka 35 na badala yake ataangalia namna nyingine ya kuwatumikia wananchi huku akigusia mchakato wa kuwania urais ambao, alisema anamwachia Mungu. “Kwa ubunge nimekwisha waeleza inatosh...

Dk Shein awasili nchini China kwa ziara ya kikazi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na ujumbe aliofuatana nao wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Beijing nchini china kwa ziara ya mualiko wa Serikali wa Jamhuri hiyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi Mdogo wa China nchini Tanzania anayefanyia kazi zake Zanzibar Bibi Chen Qiman, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Beijing nchini china kwa ziara ya mualiko wa Serikali wa Jamhuri hiyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini China,katika VIP katika uwanja wa ndege wa Beijing nchini china kwa ziara ya mualiko wa Serikali wa Jamhuri hiyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakiwa katika mapunziko mfupi katika Chumba cha Viongozi wakuu VI...

Bayern Munich yanyakua ubingwa wa Champions League

Baada ya kushinda ubingwa wa ligi ya Ujerumani, Bundesliga, kabla ya ligi hiyo kufikia mwisho na kuweka rekodi ya aina yake ya pointi, sasa Bayern Munich imetia kibindoni taji lake la tano la ubingwa wa Ulaya. Ni Arjen Robben ndiye aliyepachika bao la ushindi katika dakika ya 89 na kuipatia Bayern Munich ushindi muhimu dhidi ya mahasimu wao Borussia Dortmund jana Jumamosi (25.05.2013), baada ya mchezo wa kuvutia wa fainali ya ChampionsLeague katika uwanja wa Wembley mjini London. Wakati muda wa nyongeza ukipiga hodi, Robben alipokea pasi ya kisigino kutoka kwa Frank Ribery, akamkwepa Mats Hummels na kuuweka mpira wavuni akimwacha Roman Weidenfeller bila majibu na kuipatia Bayern Munich taji lake la tano la mabingwa wa Ulaya. Ulikuwa muda uliokuwa unasubiriwa mno kwa Bayern na Robben baada ya kushindwa kulitwaa taji hilo katika fainali za mwaka 2010 na 2012, wakati walipobwagwa kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Chelsea London katika uwanja...