Mbunifu maarufu wa mavazi kutoka Tanzania, Mustafa Hassanali ndiye Mtanzania pekee katika fani ya mitindo aliyepewa mualiko wa kushiriki katika maonyesho ya Wiki ya Mitindo Afrika chini ya African Fashion International (AFI) yatakayofanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 24-28 Oktoba, 2012 katika ukumbi wa Melrose Arch, jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini. Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya kutengeneza Magari ya Mercedes-Benz yanatarajiwa kuwashirikisha wabunifu wa mavazi zaidi ya 35 kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika, baadhi ya nchi hizo ni wenyeji Afrika ya Kusini, Ivory Coast, Morocco, Msumbiji, Cameroon, Rwanda, Angola, DRC, Nigeria, Ghana na Tanzania. “Ni maonyesho ya pekee na yenye heshima yake barani Afrika na hata duniani kwa ujumla kwani wabunifu walioalikwa ni wazoefu na bora katika fani ya Mitindo barani Afrika. Hivyo mwaliko wangu si tu utaweza kutangaza kazi ni nazofanya bali pia utasaidia kutangaza nchi yetu ya Tanzania kupitia maon...