Mfanya biashara maarufu nchini Mohamed Dewij ambaye pia ni muwekezaji katika timu ya Simba amefunguka mengi baada ya ushindi wa Simba juzi dhidi ya Mbabane kutoka nchini Swatziland ambaye kwa sasa inaitwa Eswatini. Mo Dewij ambaye ndio mara yake ya kwanza kwenda uwanjani kuangalia mpira na baada ya mchezo aliandika maneno haya:- ” Hongereni Simba kwa ushindi! Kwa kweli wachezaji wetu wamejituma. Sasa tujipange kwa mchezo wa marudiano wiki ijayo. Lengo letu ni kuwa Mabingwa wa Afrika! Isha’Allah tutafanikiwa siku moja hivi karibuni. #ThisIsSIMBA #NguvuMoja “