Waumini wa Dini ya kiislamu Mkoa wa Dar es salaam wamekumbushwa kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kutenda matendo mema
Sheikh wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhaji Mussa Salum.
Waumini wa Dini ya kiislamu Mkoa WA Dar es salaam wamekumbushwa kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kutenda matendo mema na kuepukana mambo yaliyokatazwa na Mwenyezimungu.
kauli hiyo inakuja kufuatia waislamu wote duniani kuanza kufunga mwezi mtukufu wa ramadhani ambapo kuanzia mei 17 wanajizuilia kwa kutofanya maovu,kujizuia kula na kunywa na kuacha mambo ambayo yanaenda kinyume na mwenyezimungu subhana wataala.
Kufuatia mwezi mtukufu Sheikh wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhaji Mussa Salum amesema ni vyema waumini wa kiislamu wakatambua kuwa kufunga mwezi mtukufu wa ramadhani ni ibada ambapo ni nguzo ya nne ya kiislamu.
Alhaji Salum amewaambia waislamu waepukane na dhana ya kuwa kufunga ni kujizuilia kula tu bali pia kuepukana na maovu ambayo Mwenyezimungu ameyakataza kwa muumini kuweza kuyafanya.
Amesema waislamu wanapaswa kutambua utukufu wa mwezi huu hivyo wajishughulishe katika kusoma kurani ambapo kwa mkoa huu wameandaa mashindano manne ya usomaji wa kurani yatakayofanyika ndani ya mwezi huu.
Hata hivyo Alhaji Salum ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuonyesha jitihada za kukabiliana na mapungufu ya mafuta na vyakula jambo ambalo litawaondolea shaka waislamu wakati wa mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kujipatia mahitaji Muhimu.
Mwezi mosi katika kumi la kwanza la mwezi mtukufu wa ramadhani mwezi ambao kila muislam mwenye uwezo wa kufunga anatakiwa kutekeleza ibada hii.
Mwezi mosi katika kumi la kwanza la mwezi mtukufu wa ramadhani mwezi ambao kila muislam mwenye uwezo wa kufunga anatakiwa kutekeleza ibada hii.
Comments