Skip to main content

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala yaja na ubunifu mpya ni kuhusu Choo cha mtoto wa kike

Mratibu wa Kampeni ya ujenzi  wa choo cha Mtoto wa kike ambaye pia ni Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala , Tabu Shaibu (katikati) akizungumzia maandalizi ya uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo unaotarajia kufanyika Oktoba 11 mwaka huu katika hoteli ya Lamada. Kulia ni Mwenyekiti wa kampeni hiyo na Ofisa Elimu Msingi manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas na kushoto ni moja ya wajumbe wa kampeni hiyo.


 Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam imesema
inatarajia kufanya uzinduzi wa kampeni maalumu ya ujenzi wa Choo cha mtoto wa kike Oktoba 11 kwa kuanza na shule zote za msingi katika manispaa hiyo.
  
Katika kuanzisha kampeni hiyo  mgeni rasmi katika Uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema na kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuweza kuwaunga mkono .


Akizungumza na waandishi wa habari jana Mratibu wa kampeni hiyo ambaye pia ni Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala Tabu Shaibu alisema  watumishi wanawake wa manispaa hiyo wanatambua na kuthamini jitihada kubwa za Serikali ya awamu ya tano na wadau wa maendeleo katika  kukabiliana na changamoto za mtoto wa kike na kuamua kuanzisha kampeni hiyo kama sehemu ya mchango wao.

Aidha ameeleza sababu za ujenzi wa choo cha mtoto wa kike, na kusema kuwa kila ifikapo Oktoba 11 ya kila mwaka ni siku ya Kimataifa ya Mtoto wa kike duniani na lengo la maadhimisho hayo ni kuelimisha na kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kutetea haki za mtoto wa kike.

"Tafiti zimefanyika kuhusu sababu zinazochangia mahudhurio hafifu ya mtoto wa kike darasani hasa  wa darasa la saba na takwimu zao zinabainisha wasichana wa darasa la saba hawahudhurii shuleni kati ya siku nne hadi tano kila mwezi.Vyoo visivyofaa kwa matumizi hasa kwa wasichana wanaoingia hedhi huleta changamoto kubwa kwao.


"Kutokana na changamoto hiyo watumishi wanawake wa Manispaa ya Ilala wameona wanao wajibu wa kuunga mkono juhudi za Serikali na kuendelea kuihamasisha jamii na wadau kujenga choo bora cha kisasa kitakachokuwa rafiki kwa mtoto huyu wa kike,"amesema Shaibu.
Amesema mpango huo endevu unatarajia kujenga vyoo 120 katika wilaya ya Ilala ambapo thamani ya choo kimoja ni shilingi milioni 20 .

"Manispaa yangu ipo katika kampeni endelevu ya ujenzi wa choo cha mwanafunzi wa kike katika shule za msingi  mpango huu wa choo lengo kuu kumsaidia mwanafunzi aweze kushiriki masomo katika siku nne hadi tano za mwezi"amesema 

Amesema tafiti mbalimbali zimefanyika kuhusiana na sababu mahudhurio hafifu ya mtoto wa kike darasani hususani wa darasa la saba siku tano za kila mwezi kutokana na vyoo visivyofaa kwa matumizi hasa Kwa wasichana

Amesema kila mwaka watumishi wa manispaa hiyo wameweka utaratibu wa kukutana (Kichen Paty Gala) na kuunga mkono juhudi hizo na kuendelea kuhamasisha jamii na wadau kuweza kujenga choo bora cha kisasa ambacho kitakuwa rafiki kwa mtoto wa kike ambapo kila mtumishi wa kike ameweza kuchangia shilingi, 50,000..


Kwa upande Ofisa Elimu Msingi Elzabeth Thomas amewataka wadau kuunga mkono kampeni hiyo  michango yote ielekezwe katika akaunti ya Manispaa ya Ilala Benki ya CRDB  akaunti 0150251270500 .

Elizabeti Thomas amesema kauli mbiu ya siku hiyo ni 'Binti makini Mwamvuli wangu Stara"alitolea mfano kuwa binti makini ni yule ambaye anajitambua na kujaa thamani yake kwa kuwa na maadili mazuri na hodari

Amesema uwepo wa choo cha maalum cha mtoto wa kike kitamwezesha kukaa shuleni kwa muda mrefu kushiriki masomo kikamilifu badala ya kubaki nyumbani wakati wa hedhi hali inayoathiri mtiririko wa maudhurio darasani.

"Wanafunzi wa kike wanakabiriwa na changamoto mbalimbali hii moja ya choo kama manispaa tumeimaliza tumeweza pia kujenga choo cha mfano eneo la Chanika ambacho kitazinduliwa "alisema Thomas

Pia ameongeza kuwa mwaka jana Manispaa hiyo wanafunzi watatu walikutwa na ujauzito mara baada kutokea hali changamoto hiyo ameweza kumshirikisha mkuu wa Wilaya Ilala kumaliza changamoto hiyo ya kupata mimba za utotoni.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was

HAYA NI MAKAO MAKUU YA MTANDAO WA Tigo TANZANIA DAR ES SALAAM

MAHALA yalipo ni Lugoda Street Gerezani Industrial Area , kwa sasa mdandao huu umefanya makubwa , kuna Tigo Bwerere Uilisha cheki hiyoooooo watu full kujiachia wana chonga tuu kwenye vyao vilonga.