MADEREVA wa malori wanao safirisha simenti katika kiwanda cha Nyati kilichopo nje kidogo mwa
manispaa ya kigamboni kuelekea mikoa mbali mbali wameiomba serikali kutengeneza
bara bara itokayo mwasonga hadi kibada kwa kiwango cha lami na ubora zaidi.
Madereva hao walioonekana na hali ya kutia, huruma , wengi wana wiki tatu
hadi nne wakiwa wamekwama ,hivyo kuhatarisha afya zao na hata hasara kwa siment
ambayo inanyeshewa na mvua nakupelekea kuganda nakumsababishia hasara
mfanyabiashara
Hayo yamejiri hivi karibuni gazeti hili lilipozuru eneo la tukio
nakushuhudia gari zaidi ya 60 zikiwa zimepaki barabarani zikishindwa kuendelea
na safari kutokana na ubovu wa barabara hiyo.
Mmoja wa madereva hao aliye fahamika kwa jina la Daniel Mushi kutoka
kampuni ya usambazaji ya Mvita ya jijini Dodoma, alisema yeye ni miongoni mwa
madereva waliokwama kwa takribani wiki tatu sasa huku akiwa hajui hatima yake
,amesema maisha yamekuwa magumu sana kwani mabosi hawaelewi wanachotaka nikuona
mzigo umewafikia na si vinginevyo.
“Ndugu mwandishi ombwe langu nalielekeza kwa menejiment ya kiwanda cha
nyati wao wapo ofisini wanakula upepo tuu ,lakini sisi tunateseka ,gari zao
ndiyo zinakuwa za kwanza za kwetu zinakuwa za mwisho tukifika kilometa kadhaa
tunaambiwa barabara ipo chini ya kiwango hivyo gari zeye uzito mkubwa haziwezi
kupita nyingi.Alisema,”.
Hata hivyo lawama nyingine zikawendea Mamlaka ya barabara TANROAD
kwakutotengeneza barabara hiyo kwa ubora ilihali wanaelewa kuwa mvua kubwa
zingenyesha kipindi hiki cha masika
Njia wanayotumia ni ya jeshini kwakuwa njia ya mwasonga-Kisarawe-Kibada
imefungwa ambapo wanayotumia huwalazimu kukaa siku tatu kwa umbali wa kilometa
20 tu ,serikali itupie jicho eneo hilo
Aron Michael ambaye pia ni mmoja wa madereva hao alisema kuwa Wizara ya
Viwanda inayo dhamana ya kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi viwandani ikiwemo
miundo mbinu ya barabara kwani kiwanda hicho ni miongoni mwa viwanda
vinavyoliingizia taifa fedha
“Kiwanda kikubwa kama hiki kishindwe kutengeneza kilometa 20 kwa kiwango
cha ubora,au tanroad washindwe, kilio chetu barabara itengenezwe .Alisema
Michael.
Gazeti hili linaendelea na jitihada za kuwapata watu wa tanroad ili
waweze kulitolea ufafanuzi suala hilo.
Comments